Machapisho

WELCOM TANZANIA

JEREMIA KISUBI AOMBA KUONDOKA SIMBA

Picha
CONFIRMED!! Golikipa wa Klabu ya Simba SC,Jeremiah Kisubi ameomba kuondoka kwa mkopo ndani ya Klabu hiyo kwenye Dirisha dogo la Usajili litakalofunguliwa Disemba 15 Mara baada ya kushindwa kupenya kwenye Kikosi Cha Kwanza Cha Simba na kuishia kuwa chaguo namba tatu. Kisubi ameomba kurejeshwa kwenye Klabu yake ya zamani ya Tanzania Prisons ambapo waajiri wake hao wa zamani wamemwambia kuwa wapo tayari kumlipa Mshahara robo ya ule anaopokea Simba SC kwa mda wote wa mkopo na robo tatu inayobaki wamlipe Simba. Bado hawajafikia maridhiano Kati ya Simba na Tanzania Prisons na Kila kitu kikikaa sawa Kisubi ataonekana tena Prisons kuanzia Dirisha dogo litakapofunguliwa. #wingi_van_mosesUpdates

MOO ARENA KUJENGWA KISASA

Picha
Kutoka kwa moo           "Nimepokea maoni mengi ya WanaSimba wenzangu wakishauri tujenge uwanja wetu na wako tayari kuchangia ili tufanikishe ujenzi huo.  Naomba kuweka wazi kwamba nimepokea maoni hayo kwa mikono miwili. Naomba Bodi ya Simba kukaa na kuja na utaratibu wa haraka ili jambo hili lianze utekelezaji.  Kwa Kuanza naahidi kuchangia Tsh. 2 billioni. Nawaomba wanasimba tuchange sote." Mohammed Dewji- Rais wa Heshima wa klabu ya Simba @moodewji  @simbasctanzania @wingi_van_moses

NDOA YA MTIBWA NA OMOG IMEKUFA

Picha
πŸ’₯R A S M I ✍️Klabu ya Mtibwa Sugar imeachana na Kocha Mkuu Joseph Omog πŸ‡ΈπŸ‡³ licha ya klabu hiyo kupata ushindi dhidi ya Biashara United hapo jana. Tetesi zinasema kuwa Mtibwa Sugar wana mpango wa kumchomoa Kocha Mbwana Makata kutoka kunako Klabu ya Dodoma Jiji. #@wingi_van_moses

HUYU NDO KANOUTE

Picha
​   Sadio Kanoute amekuwa ni miongoni mwa wachezaji waliozungumzwa sana baada ya mechi ya juzi dabi ya Kariakoo kati ya Simba vs Yanga, swali ni je ataendelea kutoa kile alichokitoa juzi katika mechi zijazo za Simba?. Iko hivi, uhalisia uliopo watu wengi hawamtazami Kanoute kama mchezaji mzuri anaeweza kuifanya Simba kuwa imara katika eneo la kiungo, binafsi naamini ni mchezaji mzuri ambae anahitaji muda ili kuwa bora zaidi. Kama unategemea kuona Kanoute akicheza mpira wa kukufurahisha hatakuwa mchezaji mzuri machoni mwako, yeye anatekeleza majukumu yake kimbinu na ni hapa tu ambapo watu wengi wanampa thamani ndogo kwa sababu hana mambo mengi. Ubora alioonyesha jana unaweza kuwa ni mwanzo wa kumfanya aendelee kuwa imara zaidi, kama mchezaji anaweza kucheza katika presha kubwa kama ya jana na ikapelekea azungumzwe kwa mazuri hiyo inamjenga vizuri kisaikolojia, kila la kheri kwake. #simbasctanzania #NBCPremierLeague #wingi_van_moses_ZONE

IBRAHIM AJIBU AKIONA CHA MOTO

Picha
AKIWA Rustenburg, Afrika Kusini kiungo mshambuliaji mpya wa Simba, Ibrahim Ajibu na Francis Kahata wamekiona cha moto ni baada ya Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems kutumia saa mbili sawa na dakika 120 kuwakimbiza nyota hao. Hiyo, ikiwa ni saa chache tangu timu hiyo itue Sauzi na kuweka kambi kwenye moja ya hoteli nyota tano ya Royal Marang Hotel ya nchini huko ikijiwinda na Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Bara. Ajibu alijiunga na Simba hivi karibuni akitokea Simba mara baada ya mkataba wake kumalizika wa kuichezea timu hiyo huku Kahata yeye amejiunga na timu hiyo baada ya mkataba kumalizika Gor Mahia ya nchini Kenya. Ibrahim Ajibu atakaa siku sita tu katika kambi yao ya Afrika Kusini kisha atarejea hapa na kujiunga na Taifa Stars. Meneja wa timu hiyo Patrick Rweyemamu alisema mara baada ya kutua huko juzi Jumatatu walifanya program moja ya mazoezi ya jioni kwa kutoa uchovu wa safari lakini siku iliyofuata walifanya mara mbili asubuhi na jioni. Rweyemamu alisema, programu waliyoanza...

CAF YAFANYA MABADILIKO

Picha
Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF, limetoa mwongozo mpya kuelekea michuano ya Klabu Bingwa Afrika CAFCL msimu ujao. Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya vilabu Afrika CAF imesema kuwa katika michezo ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika CAFCL na Kombe la Shirikisho CAFCC, utapigwa mchezo mmoja pekee badala ya michezo miwili. Pia mchezo huo mmoja utapigwa katika katika uwanja huru hauna uhusiano na timu yoyote kati ya zilizoingia fainali. Mabadiliko hayo yamekuja kufuatia kuzuka kwa sintofahamu katika mchezo wa pili wa fainali ya Klabu Bingwa Afrika msimu uliopita kati ya Wydad Casablanca na Esperance de Tunis, ambao haukumalizika kwa utaratibu licha ya Wydad kutangazwa mshindi na kukabidhiwa kombe na baadaye kupokonywa. Mwongozo huo mpya utazigusa timu wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Simba SC na Yanga zitakazoshiriki Klabu Bingwa Afrika, pamoja na Azam FC na KMC ambazo zitashiriki Kombe la Shirikisho endapo zitaweza kufika hatua ya fainali.

WACHEZAJIWA SIMBA WALIOBAKI DSM KWENDA BONDENI MDA WOWOTE

Picha
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Simba Sc zinasema Nyota wanne wa klabu hiyo ambao waliachwa jiji Dar Es Salaam wakati wenzao wakielekea Afrika Kusini kwenye maandalizi ya msimu mpya tayari wamekamilisha masuala ya Passport zao na muda wowote watasafiri kuwafuata wachezaji wengine. . . Nyota hao ni pamoja na Meddie Kagere, Deo Kanda, Francis Kahata na Sharaf Eldin Shoboub