SHAFFIH DAUDA AKIMBIA SIASA CHAFU DHIDI YAKE
Mkuu wa Vipindi wa Cloudsfm ambaye pia ni mdau mkubwa wa mpira wa Miguu, Shaffih Dauda ametangaza kujitoa rasmi kwenye mchakato wa uchaguzi wa TFF.
@shaffih amesema amefikia hatua hiyo baada ya kuona mbinu na siasa chafu zinazoendeshwa dhidi yake. " Mimi ni mfanyakazi wa CloudsMediaGroup, nilikwenda Mwanza kwa ajili ya kazi. Hapa Clouds tumelelewa kufanya kazi kwa bidii kufikia malengo na sitaki mambo yangu binafsi ( kugombea uongozi TFF ) kuharibu malengo ya NdondoCup na Taasisi kwa ujumla. Pia nimehangaika kutengeneza jina langu kwa miaka mingi. Natangaza kujitoa rasmi, na nitaendelea kuchangia kwenye maendeleo ya soka nchi hii nikiwa sio kiongozi " @shaffih.
Maoni
Chapisha Maoni