WAZIRI JUNIOR AWAZA KUWA MFUNGAJI BORA

Mshambuliaji mpya wa Azam, Waziri Junior amesema lengo lake ni kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.
Azam inayoendelea na maandalizi kuelekea msimu huo mpya itafungua dimba Agosti 26 kwa kucheza ugenini kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona dhidi ya wenyeji wao, Ndanda.
"Inawezekana kuwa mfungaji bora wa Ligi kikubwa ni kupigania nafasi ya kuwa nacheza katika kikosi cha kwanza, changamoto ya namba ipo popote pale ila kikubwa ni kujituma.
"Nimeanza kwa kufunga katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Lipuli, nafurahi kwa sababu nimekuwa na maelewano na wenzangu kwa muda mfupi." alisema.
Waziri amesajiliwa na Azam akitokea Toto Africans ya Mwanza iliyoshuka daraja ili kuzipa pengo la John Bocco aliyejiunga na Simba.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MBARAKA YUSUPH BADO HALI TETE

NIYONZIMA AAHIDI ZAWADI KWA KAZIMOTO