KIUNGO WA YANGA TSHISHIMBI ANAKABA HADI KIVULI
Kiungo mpya wa Yanga, Kabamba Tshishimbi ameonyesha uwezo mkubwa wa kukaba na kuanzisha mashambulizi kwa haraka katika mazoezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Polisi Kurasini, Dar es Salaam.
Yanga ilikuwa na mazoezi ya kuchezea mpira kwa kugawana vikosi vitatu ambapo katika mazoezi hayo kiungo huyo aliyesajiliwa kutoka Mbambane Swallows alionekana kutakata.
Akizungumza baada ya kumaliza mazoezi hayo Tshishimbi amesema kuwa lengo lake ni kushinda mataji akiwa na Yanga.
"Napenda kuwa mshindi siku zote, nimekuja Tanzania kushinda mataji nikiwa na Yanga hivyo nitajitahidi kuisaidia timu kwa uwezo wangu wote," alisema Tshishimbi.
Naye Andrew Vicent " Dante alimuongelea kiungo huyo na kusema ni moja ya wachezaji wazuri waliosajiliwa kipindi hiki cha usajili.
"Jamaa yupo fiti siyo mwepesi kwa maana ya kuchukua mpira mguuni kwake, kikubwa ni kushirikiana naye vizuri maana bado anahitaji muda wa kuendana na mpira wetu. " alisema Dante
Maoni
Chapisha Maoni