MANARA SASA ILE SIFA

Ofisa Habari wa Simba Haji Manara haishiwi vituko pale anapotekeleza majukumu ya klabu yake.
Ni hivi. Wakati mashabiki wa Simba wakijiuliza viongozi wao wako wapi hawaonekani uwanjani, Haji aliibuka na kuzua shangwe kwa wanazi wengi wa klabu hiyo waliofika Uwanja wa Taifa.
Haji alibebwa mkukumkuku na wanenguaji wa kundi la Msondo Ngoma na kujumuika nao kulisakata rumba.
"Pamoja na Aveva na Kaburu kuwa mahabusu lakini tukio hili limefana sana, ni dhahiri matumaini yetu mashabiki wa Simba ni kutisha kimataifa,"alisema Hamis Seif, shabiki wa Simba

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MBARAKA YUSUPH BADO HALI TETE

NIYONZIMA AAHIDI ZAWADI KWA KAZIMOTO