MWANARIADHA USAIN BOLT AFANANISHWA NA MUHAMMED ALI
Mwanariadha Usain Bolt afananishwa na Muhammed Ali
Usain Bolt ana kipaji na ana ushawishi mkubwa miongoni mwa wanariadha kama Muhammed Ali alivyokuwa na ushawishi miongoni mwa mabondia, alisema Lord Coe.
Bingwa huyo wa mbio fupi ambaye ameshinda medali ya dhabau katika michezo ya olimpiki mara nane anatarajiwa kustaafu baada ya mashindano ya ubingwa mjini London, yalioanza siku ya Ijumaa.
Coe alimfananisha raia huyo wa jamaica na mmoja wa wanamichezo mashauri duniani Muhammed Ali.
Ni bingwa wa mbio fupi duniani, alisema Coe ambaye ndiye rais wa Shirikisho la Wanariadha Duniani (IAAF).
"Usain Bolt ana kipaji, Siwezi kumfananisha na mwanamichezo mwingine yeyote yule zaidi ya Muhammad Ali ambaye amekuwa na ushawishi mkubwa nje na ndani ya michezo."
Unaweza kuanzisha mjadala kuhusu ni nani mchezaji bora wa soka duniani ama mchezaji wa tenis bora, lakini hakuna mjadala kuhusu Bolt katika mbio fupi.
Mwanariadha huyo wa Jamaica alishinda mbio za mita 100, 200 na 4 mara 100 katika michezo iliopita ya Olimpiki mjini Beijing 2008, mjini London 2012 na mjini Rio 2016.
Maoni
Chapisha Maoni