OKWI AINGIA MKATABA NA OMONG
HAPA Afrika Kusini mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi anavaa jezi namba saba huku ile namba 25 ikiendelea kuvaliwa na Shiza Kichuya na ameliambia benchi la ufundi kwamba amerudi Msimbazi kwa ajili ya kufanya kazi na wanaobisha wataona.
Okwi ambaye baada ya kuwasili Afrika Kusini alikaa na kocha wake, Mcameroon Joseph Omog kwa masaa machache na kuzungumza.
“Ninajivunia kuwa na mchezaji kama Okwi ndani ya timu kwa sababu kila mmoja anamfahamu, kipindi kile sikumwona akicheza ligi lakini sifa zake na ninavyomwona kwenye video sina wasiwasi,”alisema Omog ambaye awapo mazoezini amekuwa na msimamo na mkali kuhakikisha kazi inafanyika.
“Alipofika nimekaa na kuzungumza naye kwa masaa kadhaa, ana nidhamu na ameniahidi kufanya kazi ya maana sana na tumekubaliana jambo ambalo limefurahisha kutokana na mipango yake, ni mchezaji mkubwa anayejitambua, nasubiri kazi.”
Hata hivyo, licha ya Okwi kufanyia mazoezi jezi namba saba, huenda mchezaji huyo akarudishiwa jezi yake namba 25 ambayo kwa miaka yote imekuwa ndiyo chaguo lake kwa sababu namba hiyo inafanana na terehe aliyozaliwa.
Iko hivi, jezi hiyo namba 25 ilivaliwa na Okwi alipokuwa Simba mara ya kwanza, kwa sasa inavaliwa na Kichuya kwa takribani mwaka ingawa aliahidi angemrudishia Okwi. Hata hivyo kuna tetesi hana muda mrefu Simba, yuko njia kutimkia Misri anakohitajika.
OKWI ANENA
“Maneno mengi yamezungumzwa kuhusu mimi, watu wanaongea mengi lakini mimi ni kujiandaa vizuri, kupambana na kufanya mazoezi kwa nguvu,” alisema.
“Kikubwa ni kukaa vizuri na wachezaji wenzangu kwa sababu mpira hauchezwi na mimi peke yangu kama Okwi, hii ni timu yenye wachezaji 11 uwanjani, hivyo tutakaa pamoja na kujua tunafanya nini.
“Tuko katika maandalizi hapa Afrika Kusini, kwa ujumla ni mazuri, kambi iko vizuri na mazingira na wachezaji wana morali ya kufanya kazi.
Maoni
Chapisha Maoni