Washambuliaji wa klabu ya Azam fc "Mbaraka Yusuph" na "Shabaan Iddy"bado hawajarejea mazoezini kutokana na majeruhi waliyoyapata wakiwa na timu ya taifa huko nchini Afrika kusini. Kwa mujibu wa taarifa tulizonazo mezani kwetu" vyankende.com" ni kwamba Daktari wa Timu hiyo ameshauri wapewe muda zaidi ili kupata nafuu. Kwa sasa Azam ilikua kwenye mapumziko ya wikendi na inatarajiwa kuendelea na mazoezi leo huku ikiwa na jukumu la kucheza michezo miwili ambapo mmoja ni dhidi ya Ruvu shooting na wa pili ni dhidi ya Mtibwa Sugar
Niyonzima aahidi zawadi kwa Kazimoto Nyota mpya wa Simba aliyesajiliwa hivi karibuni baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga, Haruna Niyonzima ameahidi kumtafutia zawadi kiungo mkongwe wa klabu hiyo, Mwinyi Kazimoto kutokana na hatua yake ya ‘kumvulia jezi. Kazimoto aliyekuwa akivaa jezi namba 8, ameamua kumuachia kiungo huyo raia wa Rwanda baada ya kuombwa kufanya hivyo kama ishara ya heshima kwake. “Namshukuru sana Mwinyi kwa heshima aliyonipa, na mimi namuahidi kumtafutia zawadi, ni lazima nimzawadie kwa hili alilonifanyia” amesema Haruna Akizungumzia sababu za kuiomba jezi hiyo, Haruna ambaye mara nyingi hucheza kama kiungo namba 8, amesema jezi hiyo ina kumbukumbu kubwa katika maisha yake ya soka, na ndiyo aliyokuwa akiivaa wakati akiwa Yanga Niyonzima ambaye ameanza kuonyesha cheche katika klabu ya Simba kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Rayon Sports iliyopigwa jana kuadhimisha Simba Day, ameahidi kuitumikia Simba kwa nguvu zote katika mechi zote na amesema ataanza na m...
Maoni
Chapisha Maoni