WAAMUZI SIMBA NA YANGA HAWA HAPA
Waamuzi Simba na Yanga hawa hapa
23 Aug 2017, 09:05 am| By TANZANIA
Kuelekea pambano la ‘Ngao ya Jamii’ kati ya watani wa jadi Yanga na Simba litakalochezwa leo Jumatano uwanja wa Taifa, Dar es salaam, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza waamuzi watakaochezesha pambano hilo kali na la kusisimua.
Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amewataja waamuzi hao kuwa ni Elly Sasii atakayesimama katikati, akisaidiwa na Fernand Chacha pamoja na Hellen Mduma, huku mwamuzi wa nne (4th Official akiwa ni Israel Mujuni Nkongo)
Amesema waamuzi hao wote waliopewa jukumu la mchezo huo wana beji za FIFA kutokana na uzito wa mchezo wenyewe.
Pia, Lucas amesema mechi hiyo imesogezwa mbele ambapo muda wa kuanza kwake sasa utakuwa ni saa 11:00 jioni badala ya saa 10:00 jioni iliyokuwa imepangwa awali.
Takriban askari polisi 300 wakiwemo askari wa farasi watakuwepo uwanjani kuhakikisha ulinzi na usalama ambapo Lucas amewaonya wote wenye nia mbaya na wenye vurugu kutokanyaga uwanjani hapo
Maoni
Chapisha Maoni