KAMA unaishangaa Simba kusajili kikosi kizima na wachezaji wa akiba juu, Mbeya City nayo inapita mulemule ambapo jana Alhamisi ilitangaza majina 23 ya wachezaji ambao watakuwa nao msimu ujao ba bado wakisisitiza kuwa bado watasajili wachezaji wengine watano wapya. Zikiwa zimebaki siku 10 kabla ya dirisha la usajili kufungwa, Kaimu Ofisa Habari wa Mbeya City, Shaa Mjanja, alisema kuwa licha ya timu hiyo kufanya usajili wa wachezaji zaidi ya watano wapya, bado hawajafunga zoezi hilo na kabla ya wiki hii kumalizika watawatambulisha wachezaji wengine. Shaa alisema kikosi kipo kambini, lakini kutokana na ripoti ambayo ilipendekezwa na benchi la ufundi wanatakiwa kusajili wachezaji wengine watano ili kuwa tayari kwa mapambano ya msimu ujao. Wachezaji hao ni, Fikirini Bakari, Majaliwa Shabani, Hassan Mwasapile, Hamisi Msabira, Ally Lundenga, Erick Kiaruzi, Babu Ally, Issa Selemani, Rajabu Isihaka, John Kabanda, Danny Joram, Frank Hamisi, Sankan Mkandawile, Owen Chaima, Mrisho Ngassa, Medso...