Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 29, 2017

PRISON MABINGWA KOMBE LA HISANI YAIPIGA YANGA 3-1

Picha
Picha kwa hisani ya BIN ZUBERY Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania, Godfrey Simbeye, akimkabidhi Kombe, Nahodha wa timu ya Tanzania Prisons, Laurian Mpalile, baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Yanga U20 katika mchezo wa Hisani wa fainali wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS, Dk. Leonard Maboko (kulia kwake) ni Katibu wa TFF Mkoa wa Mbeya, (kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS, Elizabeth Kaganda. Kiungo wa Yanga B, Said Mussa (kushoto) akiudhibiti mpira mbele ya mchezaji wa Tanzania Prisons, Mohamed Rashid kwenye mchezo huo   Beki wa Tanzania Prisons, James Mwasote akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga B, Samuel Greyson  Mshambuliaji wa Yanga B, Festo Geryson (kushoto) akiwania mpira wa juu na beki wa ...

JIUNGE NA GROUP LA WHATSUP TWENDE KISPORT TZ

Picha
Follow this link to join my WhatsApp group: https://chat.whatsapp.com/I4W5gyXLFIx8d4PK1DL9gn

MBARAKA YUSUPH BADO HALI TETE

Picha
Washambuliaji wa klabu ya Azam fc "Mbaraka Yusuph" na "Shabaan Iddy"bado hawajarejea mazoezini kutokana na majeruhi waliyoyapata wakiwa na timu ya taifa huko nchini Afrika kusini. Kwa mujibu wa taarifa tulizonazo mezani kwetu" vyankende.com" ni kwamba Daktari wa Timu hiyo ameshauri wapewe muda zaidi ili kupata nafuu. Kwa sasa Azam ilikua kwenye mapumziko ya wikendi na inatarajiwa kuendelea na mazoezi leo huku ikiwa na jukumu la kucheza michezo miwili ambapo mmoja ni dhidi ya Ruvu shooting na wa pili ni dhidi ya Mtibwa Sugar

MICHO AVUNJA MKATABA NA UGANDA CRANES

Picha
Namwandishi wetu WINGIASA MOSES: KOCHA Mserbia, Milutin Sredojevic ‘Micho’ ameuvunja mkataba na Shirikisho la Soka Uganda (FUFA) kufundisha timu ya taifa ya nchi hiyo, The Cranes kutokana na kutolipwa malimbikizo ya mishahara yake hadi kufika dola za Kimarekani 64, zaidi ya Sh. Milioni 140 za Tanzania.  Micho ambaye Septemba 1, mwaka huu atafikisha umri wa miaka 48 ameiambia Twende Kisport Tz Blog leo kwa simu kutoka Uganda kwamba amelazimika kuondoa The Cranes baada ya uongozi wa FUFA kutothamini mchango wake na kushindwa kumlipa kwa muda mrefu.  “Nimevunja mkataba kutokana na kutolipwa mishahara yangu, nimetuma taarifa ya kuvunja mkataba FUFA na kumpa wakala wangu jukumu la kukamilisha taratibu za kuachana nao,”amesema Micho. Kocha Mserbia, Milutin Sredojevic 'Micho' akizungumza na Waandishi wa Habari leo Micho anaondoka Uganda baada ya miaka minne, akijivunia kuiwezesha The Cranes kurejea kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) Januari mwaka huu nchini ...

SIMBA B YATUPWEA NJE MASHINDANO YA HISANI MBEYA

Picha
TIMU ya Vijana wa Simba chini ya umri wa miaka 20, jana walishinda kuungana na wenzao wa Yanga katika fainali ya Mechi za Hisani kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI baada ya kufungwa na Tanzania Prisons kwa mikwaju ya penati 6-5 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu wa Sokoine jijini Mbeya. Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu zote kutoka uwanjani bila kupata bao, huku timu zote zikicheza kwa taadhari na kufanya mashambulizi ya kushitukiza. Katika mchezo huo Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 69 kupitia kwa mshambuliaji wake, Dadi Mbarouk, baada ya kuwatoka mabeki wa Tanzania Prisons Aron Kalambo, aliyekuwa ametoka golini akijaribu kuwahi kumzuia na  kupishana na mpira uliotinga wavuni. Mshambuliaji wa Tanzania Prisons B, Mohamed Rashid akimyoka beki wa Simba B, Jacob Jalala (kulia) jana Bao la kusawazisha la Tanzania Prisons, lilifungwa na Kassim Hamis, kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 79, baada ya mchezaji wa Simba U20, kuunaw...

KURASA ZA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI 30/07/2017

Picha
Kurasa za magazeti ya leo jumapili,30 julai 2017 Published Under  NEWSPAPER Magazetini leo Jumapili Julai 30,2017 The Sunday People has an interview with Kerry Katona... Ant McPartlin is set for a return to television, reports the Sunday Mirror... Donald Trump is losing support in his Republican party after a week of turmoil, says The Observer... A woman who was forced to travel to Syria by her jihadist husband has told The Sunday Times about the Islamic State "Little Britain" she shared with British teenagers who had fled home to join the so-called "caliphate"... Chancellor Philip Hammond's push for a transition before Brexit takes effect has been criticised by a key ally of Foreign Secretary Boris Johnson, reports The Sunday Telegraph... Princess Diana's brother Earl Spencer has pleaded with Channel 4 not to broadcast his sister's "video diaries", according to The Mail on Sunday...

MBWANA SAMATTA "CHAMPION BOY" AFUNGUA KITABU CHA MAGOLI

Picha
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ‘Champion Boy’ ameuanza msimu mpya wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji kwa kufunga katika sare ya 3-3 na Waasland-Beveren Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk. Waasland-Beveren waliuanza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kuongoza kwa mabao 2-0 hadi baada ya mapumziko wafungaji Olivier Myny dakika ya 45 na Zinho Gano dakika ya 47. Lakini Genk wakazinduka na kukomboa mabao hayo kupitia kwa Jose Naranjo dakika ya 70 na  Samatta dakika ya 80 kabla ya Mtanzania huyo kumsetia Siebe Schrijvers kufunga bao la tatu dakika ya 82. Mbwana Samatta (kushoto) akikimbia na wenzake baada ya kuisawazishia Genk na kuwa 2-2 kabla ya mchezo kumalizika kwa sare ya 3-3 Mbwana Samatta (juu kulia) akipambana katika mchezo huo uliokuwa mkali  Hata hivyo, wakati Genk wakiamini wataondoka na pointi tatu, wakajikuta wanachomolewa bao dakika ya mwisho ya mchezo, baada ya Zinho Gano tena kuifungia Waasland-Beveren dakika ya 90 na ushei....

AZAM YAMSAJIRI KIPA WA GHANA ALIYEDAKA CHAN

Picha
AZAM FC imejiimarisha baada ya kumsajili kipa Razak Abalora mwenye umri wa miaka 20, kutoka klabu ya WAFA SC ya Ghana kwa mkataba wa miaka mitatu. Abalora mwenye rekodi ya kudaka mechi 12 mfululizo bila kuruhusu nyavu zake kuguswa katika mechi 22 msimu huu, anaondoka kwa washindani wa taji la Ligi Kuu ya Ghana baada ya msimu mwingine mzuri kwake. Alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ghana ya wachezaji wa nyumbani pekee, inayojiandaa na mchezo ujao wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) dhidi ya Burkina Faso. Meneja Mkuu wa Azam FC, Abdul Mohammed (kushoto) akimkabidhi jezi kipa mpya, Razak Abalora kutoka WAFA SC ya kwao, Ghana  Na Razak Abalora anaondoka wakati vigogo wa Ghana, Hearts of Oak walikuwa wanajipanga kuzungumza na WAFA ili wamnunue a Razak Abalora. Abalora moja kwa moja anakwenda kuwa kipa namba moja wa Azam FC akichukua nafasi ya Aishi Manula anayehamia Simba SC. Abalora anakwenda kufanya idadi ya makipa wanne wa kiko...

METHOD MWANJALI NAHODHA MPYA SIMBA

Picha
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. ______________  Benchi la ufundi la klabu ya Simba,chini ya kocha wake mkuu Joseph Omog limefanya marekebisho kwenye eneo la unahodha wa timu.  Katika marekebisho hayo yaliyoridhiwa na uongozi wa klabu,beki wa kimataifa Mzimbabwe Method Mwanjale ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa timu ya Simba,akichukua nafasi ya Jonas Mkude atakaendelea kuwa mchezaji mwandamizi kwenye kikosi hicho,ambacho kwa sasa kipo nchini Afrika kusini kujiandaa na msimu mpya unaotarajiwa kuanza mwezi ujao.  Kwenye mabadiliko hayo ya kawaida, benchi la ufundi pia limewateua Mchezaji bora wa ligi kuu ya Tanzania na klabu ya Simba kwa msimu huu,Mohammed Hussein(Tshabalala)na John Raphael Boko kuwa manahodha wasaidizi wa timu hiyo.  Klabu inamshukuru sana Nahodha wake kwenye msimu uliopita na mchezaji wake mwandamizi,Jonas Mkude kwa kazi nzuri alioifanya muda wote alipokuwa Nahodha wa Timu.  Kwa sasa kikosi chetu kinaendelea na mazoezi na kila kitu kinakwenda ...

TETESI ZA USAJIRI BARANI ULAYA LEO HII JUMAMOSI

Picha
Saa 2 zilizopita Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionNaymar kujiunga na PSG Mshambuliaji wa Barcelona Neymar, 25, amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano kujiunga na Paris Saint-Germain na huenda akakamilisha uhamisho wa pauni milioni 197 wiki ijayo. (RMC) PSG watawapa Barcelona Angel Di Maria, 29, kama sehemu ya mkataba wa kumsajili Neymar, ili kupunguza kodi ya kutengua kifungu cha uhamisho cha mchezaji huyo wa Brazil. (AS) Iwapo Neymar ataondoka, Barcelona wataamua kuwawinda wachezaji watatu kutoka EPL- Philippe Coutinho, 25, wa Liverpool, Eden Hazard, 26, wa Chelsea, na Delle Alli, 21 wa Tottenham kuziba pengo. (Mirror) Image captionPhillip Coutinho Barcelona wana wasiwasi kuwa bei kubwa ya kumsajili Philippe Coitinho kutoka Liverpool huenda ikawakatisha tamaa. (AS) Kiungo wa Barcelona Andres Inisesta, 33, amesema ni Neymar pekee anayeweza kuzungumzia kuhusu hatma yake, akisema hadhani kama euro milioni 200-300 zina manufaa yoyote kwa klabu bila Neymar mwenyewe. (Marca...

BAADA YA ZILE NDUNDI NEYMA AREJEA MAZOEZINI

Picha
Baada ya kuzichapa na beki mpya wa Barcelona, Nelson Semedo , mshambuliaji Mbrazil, Neymar amerejea mazoezini. Barcelona bado iko Miami nchini Marekani na Neymar alitoka mazoezini kwa hasira baada ya ugomvi huo jana. Baadaye ikaelezwa hatarejea Hispania na Barcelona na yuko katika mpango wake wa kutaka kuondoka kujiunga na PSG ambayo inamtaka kwa udi na uvumba. Hata hivyo, leo amerejea mazoezini lakini akionekana ni mtu asiye na furaha.

YULE RASTA WA YANGA AMERUDI KWAO

Picha
Kiungo mkabaji wa Mbabane Swallows ya Swaziland, Papy Kabamba Tshishimbi, jana asubuhi aliondoka nchini kurudi kwao DR Congo, lakini ameiachia mzigo mzito Yanga iliyofikia makubaliano naye ya kumsajili. Hali hiyo, imekuja ikiwa ni siku chache tangu kiungo huyo atue nchini na kufanya mazungumzo na Yanga kwa ajili ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja waliokubaliana naye. Tshishimbi raia wa DR Congo, tayari amefanyiwa vipimo vya afya na Yanga ambavyo vimeonyesha amefuzu, hivyo yupo kamili kwa ajili ya kuichezea timu hiyo bingwa wa Ligi Kuu Bara. Taarifa za kuaminika kutoka Yanga zinaeleza, kiungo huyo amemalizana kila kitu na klabu hiyo lakini kilichobaki ni Yanga kumalizana na Mbabane kwani Tshishimbi bado ana mkataba nao wa miezi minne. Imeelezwa kuwa, kiungo atarejea nchini kujiunga na Yanga mara baada ya pande hizo mbili kumalizana katika mkataba wake wa miezi minne aliyoibakisha Mbabane. Yanga imedai makubaliano na Mbabane yatafikiwa muafaka hivi karibuni kutokana na klabu hiyo ya ...

BAADA YA NDEMLA KWENDA SWEEDEN KICHUYA NAYE ANUKIA MISRI

Picha
Siku chache baada ya kiungo wa Simba, Said Ndemla kwenda Sweden kufanya majaribio katika Klabu ya AFC, mshambuliaji wa timu hiyo, Shiza Kichuya anaweza akapata shavu la kucheza soka nchini Misri. Taarifa kutoka ndani ya Simba zinasema klabu moja ya Misri inamtaka Kichuya ili imsajili kwa ajili ya kuichezea timu yao na sasa wapo katika mazungumzo. Bado mazungumzo ya Simba na klabu hiyo yanaendelea na wakifikia muafaka muda wowote Kichuya ataondoka kwenda nchini humo. “Kuna timu ya Misri kupitia wakala aliyemuona Kichuya kwenye ligi na kufanya mawasiliano na sisi na tayari kuna barua wameleta wakimtaka Kichuya. “Kuna dau ambalo wamelipendekeza ili waweze kumsajili Kichuya lakini sisi hatujakubaliana nalo, hivyo tupo katika mazungumzo ya kuweza kufikia makubaliano lakini tunataka waongeze dau. “Hata hivyo, itabidi tumuachie Kichuya akacheze soka la kulipwa kwani kumzuia mchezaji kwa sasa ni sawa na bure, kwani amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na hatutaki baa...