Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 30, 2017

RAPHAEL DAUDI LOTH RASMI MARI YA YANGA

Picha
Na Zepha da silver, DAR ES SALAAM YANGA SC imefanikiwa kukamilisha uhamisho wa kiungo chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Raphael Daudi Loth kutoka Mbeya City. Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika amesema kwamba kiungo huyo wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesaini mkataba wa miaka miwili kuhamia timu ya Dar es Salaam. “Tunafurahi kuwatangazia wana Yanga kwamba tumefanikiwa kukamilisha usajili wa kiungo wa Raphael Daudi kutoka Mbeya City ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili,”amesema. Raphael Daudi Loth akisaini mkataba wa miaka miwili Yanga SC kutoka Mbeya City Na Daudi anakuwa mchezaji wa nane mpya kusajiliwa Yanga SC katika dirisha hili hadi sasa, baada ya makipa Mcameroon Youth RostandE kutoka African Lyon iliyoshuka Daraja, Ramadhan Kabwili aliyepandishwa kutoka timu B, beki Abdallah Hajji kutoka Taifa Jang’ombe, viungo Pius Buswita kutoka Mbao FC, Papy Kabamba Tshishimbi, Mkongo kutoka Mbabane Swallows ya Swaziland, Hussein Akilimali huru na ms...

LACAZETTE AFUNGA LAKINI ARSENAL YAPIGWA 2-1 KOMBA LA EMIRATES

Picha
LACAZETTE AFUNGA LAKINI ARSENAL YAPIGWA 2-1 KOMBE LA EMIRATES Mshambuliaji mpya wa Arsenal, Alexandre Lacazette akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao dakika ya 62 katika kipigo cha 2-1 kutoka kwa Sevilla kwenye mchezo wa Kombe la Emirates, Uwanja wa Emirates mjini London. Mabao ya Sevilla yamefungwa na Joaquin Correa dakika ya 49 na Steven N'Zonzi dakika ya 69

DAN ALVES AWAPIKU MESS NA RONALDO KWA RECORD

Picha
Mkongwe wa zamani wa Manchester United Ryan Giggs na mkongwe wa zamani wa Liverpool Kenny Danglish walikuwa na rekodi ya kuwahi kubeba vikombe vingi duniani ambapo kila mmoja alikuwa na makombe 35. Rekodi hii imekuwa ngumu sana kufikiwa na hata wachezaji wakubwa wawili duniani Lioneil Messi na Cristiano Ronaldo wameshindwa kuvunja au kufikia rekodi waliyokuwa nayo Danglish na Giggs. Ryan Giggs alipata makombe yote hayo akiwa na Manchester United huku Danglish akichukua makombe hayo 14 akiwa na Celtic na 21 yaliyobaki aliyachukua akiwa na klabu yake ya Livepool. Lakini hapo jana mlinzi wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Brazil Dani Alves alivunja rekodi hiyo ya wakongwe hao wawili baada ya kuisaidia klabu yake hiyo mpya kubeba ubingwa wa French Super Cup. Alves ameshawahi kushinda kombe 1 akiwa na Bahia, akashinda 3 akiwa na Brazil, akashinda 2 akiwa na Juventus, akashinda 5 akiwa na Sevilla huku akishinda jumla ya makombe 23 akiwa na Barcelona na kumfanya ashinde jumla ya makombe...

NEMANJA MATIC ANAKWENDA MAN U

Picha
Kiungo Nemanja Matic amefuzu vipimo na muda mchache atatangazwa kuwa mchezaji rasmi wa Man United. Matic anatoka Chelsea kujiunga na Man United kwa mkataba wa thamani ya pauni million 31. Raia huyo wa Serbia amekuwa chaguo namba moja la Kocha Jose Mourinho tokea akiwa Chelsea na sasa ametua Man United amefanya juu chini kuhakikisha anamnasa

SOMA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU 31.07.2017

Picha
Haya Hapa Magazeti Yote Ya Leo Jumatatu Ya tarehe 31 July 2017  wingiasa moses Monday, July 31, 2017   Magazeti ,          

MSUVA AFUNGUA KITABU CHAKE CHA MAGOLI MOROCCO

Picha
Mshambulizi mpya wa Difaa Al Jadid, Simon Msuva ameanza vizuri kwa kufunga bao safi. Timu hiyo inashiriki Ligi Kuu ya Morocco. Msuva ameanza kwa kufunga bao katika mechi ya kirafiki waliyocheza leo ingawa Difaa Al Jadid walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1. “Kweli nimefunga bao moja ingawa tumepoteza, namshukuru Mungu nimeanza vizuri,” alisema Msuva ambaye amejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu. Msuva alitua nchini humo siku nne zilizopita kabla ya kusaini mkataba na kuanza mazoezi moja kwa moja

MESSI NA MSUVA WALIVYOPIGA KAZI LEO

Picha
Kiungo Mtanzania, Ramadhani Singano 'Messi' akiichezea timu yake mpya, Difaa Hassan El Jadida mchezo wa kirafiki leo nchini Morocco Winga Mtanzania, Simon Msuva naye alipangwa kwa mara ya kwanza Difaa Hassan El Jadida baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI 30.07.2017

Picha
TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI 30.07.2017 Baba yake Neymar ameiomba PSG kusubiri kuanza mazungumzo rasmi ya uhamisho wa pauni milioni 450 wa mwanae hadi baada ya Julai 31, tarehe ambayo atapata bakshishi yake ya pauni milioni 23.3 kutoka kwa Barcelona ya kumshawishi Neymar kusaini mkataba mpya mwaka jana Oktoba. (Sunday Times) Barcelona watawashtaki Paris Saint-Germain kwa UEFA kwa kukiuka kanuni za fedha (FFP) iwapo PSG watatoa dau la pauni milioni 197 kutengua kifungu cha usajili cha Neymar. (ESPN) Iwapo Neymar, 25, ataondoka Barcelona na kujiunga na PSG, Barca huenda wakaamua kumchukua mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoinne Griezmann, 26 kuziba pengo. (Marca) PSG wakikamilisha usajili wa Neymar, watapanda dau la pauni milioni 35 kumtaka mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez, 28 kutoka Arsenal. (Sunday Express) Philippe Coutinho, 25, atamuomba meneja wa Liverpool Jurgen Klopp kumruhusu ajiunge na Barcelona. Iwapo Coutinho ataondoka, Klopp atataka kumsajili winga wa Borussia D...

"SIMBA WEEK" KUTINGA TAASISI YA MOYO YA JK

Picha
Maadhimisho ya siku maalum ya klabu ya Simba maarufu kama ‘Simba Day’ yanaanza siku ay Jumanne Agosti 01, 2017 na yatakwenda wiki nzima hadi Agosti 8 ambaye ndiyo siku ya kilele. Katika wiki hiyo itakayofahamika kama ‘Simba Week’, uongozi wa klabu hiyo kwa kushirikiana na mashabiki pamoja na wachezaji wanatarajiwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii, ambapo kwa mwaka huu, moja ya shughuli zitakazofanyika ni kuchangia matibabu ya upasuaji wa kwa watoto wenye matatizo ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Muhimbili Jijini dar es Salaam. Mratibu wa shughuli hiyo Imani Kajula amesema mbali na kuchangia upasuaji huo, pia viongozi na wachezaji watatembelea taasisi hiyo kubwa ya moyo barani Afrika ndani ya ‘Simba Week’ Pia amesema miongoni mwa shughuli nyingine za kijamii itakuwa ni kutoa misaada malimbali kwa watoto yatima katika vituo vitakavyobainishwa hapo baadaye. Kauli mbiu ya Simba Day mwaka huu ‘Ki-Simba zaidi’, ...

MSUVA AJIPANGA KUPAMBANIA NAMBA MOROCCO

Picha
Baada ya kukamilisha uhamisho wa kujiunga na klabu ya Difaa Al Jadida ya Morocco, mshambuliaji Simon Msuva amesema nchi hiyo ni njia ya kuelekea barani Ulaya. Mshambuliaji huyo alisaini mkatana wa miaka mitatu wa kuichezea Jadida, mkataba ambao unahitimisha miaka mitano ya kuichezea Yanga aliyojiunga nayo 2012 akitokea Moro United ya Morogoro. Mwananchi kupitia vyanzo vyake mbalimbali, linafahamu kuwa Msuva amesajiliwa kwa dau la zaidi ya 200 milioni za Tanzania. Akizungumza na MCL Digital baada ya kusaini mkataba huo, mchezaji huyo alisema hiyo ni fursa kubwa kwenye maisha yake ya soka. “Mimi ni mchezaji ninayejiamini na hata kufika hapa ni kutokana na kupambana, ninaamini milango zaidi itafunguka kutoka hapa, nimeanza maisha mapya. Jukumu langu ni kufanya kazi kwa bidii,” alisema Msuva. Hata hivyo mfungaji huyo bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2018/17 alisema haitakuwa kazi rahisi kwake kupata nafasi ya kuanza kikosini. “Itakuwa ngumu kupata nafasi, lakini niko t...