Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 31, 2017

TFF KUZIPUNGUZIA MZIGO SIMBA NA YANGA

Picha
Dar es Salaam. Kamati ya utendaji ya shirikisho la soka Tanzania (TFF), imezipunguzia mzigo za Ligi Kuu baada ya kuridhia kupunguza ada inayolipwa kwa wachezaji wa kigeni wanaosajiliwa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF leo, kila mchezaji wa kigeni anayesajiliwa na klabu inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara sasa atalipiwa ada ya Shilingi milioni mbili tofauti na hapo awali ambapo kanuni ilitaka kila mchezaji wa kigeni alipiwe ada ya Dola 2000 (Sh.4.5 milioni). Mabadiliko mengine ya kanuni ambayo kamati ya utendaji ya TFF imeyaridhia ni kutotambuliwa kwa mkataba wa mchezaji ambao haujasajiliwa na shirikisho hilo sambamba na wachezaji kukatiwa bima za afya. Masharti hayo ni kukatiwa Bima ya Matibabu, Kuidhinishwa afya yake ambayo mara baada ya fomu yake kupitishwa na Kamati ya Tiba ya TFF kwa mujibu wa Kanuni ya 18 (1) ya Ligi Kuu na Mkataba wake wa maandishi ‘hardcopy’ kuwasilisha TFF kwa mujibu wa Kanuni ya 69 (8) ya Ligi Kuu. Kama kuna timu haitakidhi japo sharti ...

UMEMSIKIA HAJI MWINYI {ETI SAUZI KAMA MORO TU}

Picha
Morogoro. WAKATI Simba, wakitambia uwepo wao Afrika Kusini, beki wa Yanga, Haji Mwinyi hajaumizwa na hilo kwa madai sehemu walikojichimbia hapa Morogoro ni kama Sauzi tu. "Afrika Kusini kwa sasa kuna baridi kali,huku Morogoro tupo maeneo ya Mlimani ambapo baridi lake ni kali mno, uwanja ni mzuri ambao unatufanya tuwe na maandalizi ya aina yake, ndiyo maana nimesema Sauzi ni kama Morogoro tu,"alisema Alielezea kwamba kinachotakiwa ni kujiandaa vya kutosha na siyo umarufu wa sehemu kwa madai matunda ya kambi hizo yataonekana uwanjani na siyo maneno ya mitaani. "Mwisho wa yote zote ni kambi tu, ila cha kuzingatia katika kambi hizo kinafanyika kitu gani cha kufanya timu iwe na maendeleo yanayotakiwa,mfano sisi baridi la huku linatufanya tufanye mazoezi kwa muda mrefu bila kuchoka,"alisema Alitolea mfano pindi Simba, ilipokuwa chini ya Dylan Kerr,ambaye kwa sasa anaifundisha Gor Mahia ya Kenya, kwamba waliweka kambi Lushoto ambako kuna baridi ambalo liliwasaidia kuji...

PATA RATIBA ZA TIMU KUBWA TANO ZA ENGLAND

Picha
ZIMEBAKI SIKU CHACHE LIGI KUU PENDWA KUFUNGULIWA YAANI LIGI YA ENGLAND     NIMEKUSOGEZEA RATIBA KAMILI ZA TIMU KUU TANO ZA ENGLAND

MAGAZETI YA LEO JUMANNE 01.08.2017

Picha
Makubwa ya Magazeti ya TZ leo August 1.. Udaku, Michezo na Hardnews Ni asubuhi nyingine tena nakukutanisha na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania leo August 1  2017  kuanzia ya Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa.

SIMBA KUTESTI MITAMBO SIKU YA LEO

Picha
Johannesburg,Afrika Kusini. MABINGWA wa kombe la FC,Simba SC leo Jumanne wanatarajiwa kucheza mechi yao ya kwanza ya maandalizi ya msimu mpya kwa kuvaana na mabingwa wa zamani wa Afrika,Orlando Pirates ya Afrika kusini.  Orlando Pirates ambayo ndio klabu maarufu zaidi nchini humo,imeahidi kushusha silaha zake zote muhimu ili kuwapa maandalizi ya kutosha Simba SC.Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye dimba la Orlando liliopo jijini Johannesburg.  Mechi nyingine ya mwisho itakayochezwa na Simba SC nchini humo itapigwa siku ya Alhamisi ya wiki hii dhidi ya mabingwa wa soka nchini humo kwa sasa Bidvest Wits wanaochezewa na kiungo wa zamani wa Everton na Sunderland, Steven Piennar. Wakati huohuo Simba SC wamethibitisha kumsajili mlinda mlango Aishi Manula kutoka Azam FC kwa mkataba wa miaka miwili. Mlinda mlango huyo anayeichezea pia timu ya taifa ya Tanzania,kesho Jumanne ataungana na wachezaji wenzake walioweka kambi huko Eden Vale Johannesburg, nchini Afrika kusini....

AISHI MANURA KUJIUNGA NA SIMBA TAREHE 01.08.2017

Picha
Golikipa wa kimataifa wa Tanzania Aishi Salum Manula kesho tarehe moja,anatarajiwa kujiunga rasimi na kambi ya klabu yetu ya Simba iliopo Eden Vale Johannesburg, nchini Afrika kusini. Manula ambae ndio Golikipa namba moja wa nchi hii ameshamalizana kila kitu kuhusu kujiunga na klabu yetu,na ameahidi kuwapa furaha wanachama na washabiki wetu,sambamba na kuisaidia klabu kushinda mataji itakayowania msimu huu. Wakati huo huo kesho timu ya Simba inatarajiwa kucheza mechi ya kwanza ya maandalizi ya msimu dhidi ya mabingwa wa zamani wa Afrika Orlando Pirates ya nchini Afrika kusini. Orlando ambayo ndio klabu maarufu zaid nchini humo,imeahidi kushusha silaha zake zote muhimu ili kuwapa maandalizi ya kutosha Simba,Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye dimba la Orlando liliopo jijini Johannesburg. Mechi nyingine ya mwisho itakayochezwa na Simba nchini humo itapigwa siku ya Alhamis ya wiki hii dhidi ya mabingwa wa soka nchini humo kwa sasa Bidvest Mwisho klabu ya Simba kesho inawaalika w...

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU 31.07.2017

Picha
TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU 31.07.2017 Jose Mourinho amesema Nemanja Matic, 28, “anataka sana” kuondoka Chelsea na kujiunga na Manchester United. Tayari United wamekubali kutoa pauni milioni 40 na wanatarajia kukamilisha usajili huo siku chache zijazo. (Sky) Beki wa kulia wa Paris Saint-Germain Serge Aurier amekubali kujiunga na Manchester United, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ufaransa. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ameruhusiwa kuondoka na meneja Unai Emery. (Sky Sports) Alexis Sanchez anafikiria kuwasilisha ombi la kuondoka Emirates ili kulazimisha uhamisho wake kwenda Manchester City. Sanchez anataka sana kuondoka, na Pep Guardiola yuko tayari kufanikisha usajili wake. Sanchez anataka mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki, na Arsenal wako tayari kutoa 300,000. (Daily Mirror) Southampton wana matumaini kuwa Virgil van Dijk atabadili mawazo na kurejea mazoezini na kikosi cha kwanza wiki hii. Southampton hawataki kumuuza beki huyo anayenyatiwa na Liverpool. (Dai...

KESI ZA AKINA MALINZI, AVEVA,KABURU ZAAHIRISHWA TENA LEO KISUTU

Picha
KESI ZA AKINA MALINZI, AVEVA, KABURU ZAAHIRISHWA TENA LEO KISUTU Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM KESI inayowakabili viongozi wakuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Rais Jamal Malinzi na Katibu weke, Selestine Mwesigwa imeahirishwa tena hadi Agosti 11, ili kupisha upepelezi zaidi. Mapema hii leo, wawili hao pamoja na Mkurugenzi wa Fedha wa TFF, Isinde Isawafo Mwanga walifikishwa tena mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu mjini Dar es Salaam, hiyo ikiwa ni mara ya nne na kusomewa mashitaka yao 28, kabla ya kesi hiyo kupelekwa tena mbele hadi Julai 31. Hakimu mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbroad Mashauri, alisema anaiahirisha kesi hiyo tena kwa sababu upelelezi haujakamilika na washtakiwa wanarudi rumande hadi Agosti 11 kesi hiyo itakapotajwa tena. Malinzi, pamoja na Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa na Mhasibu, Nsiande Isawafo Mwanga walipelekwa rumande Juni 29 baada ya kusomewa mashitaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF iliyopo katika banki ya Stanbic, Da...

MASTAA WA SIMBA WAFUNGUKA MKUDE KUPOKWA UNAHODHA

Picha
Taarifa za uongozi wa timu ya Simba pamoja na benchi la ufundi chini ya kocha mkuu Joseph Omog kumvua unahodha kiungo wake wa kutumainiwa Jonas Mkude limeendelea kuzua mjadala ambapo nahodha wa zamani wa timu hiyo, Henry Joseph amefunguka. Henry Joseph maarufu kwa jina la 'Shindika' ameongea na gazeti hili kutokea nchini Norway ambapo alisema wazi kuwa timu hiyo imefanya jambo lisilo la kiungwana kulinganisha na kazi yake aliyoifanya ndani ya timu hiyo. Shindika alisema kiungo huyo hata kama alikuwa na makosa binafsi lakini sio sababu ya yeye kuvuliwa jumla uongozi huo badala yake ilipaswa angalau apewe unahodha msaidizi ambapo alishauzoea. "Kiukweli mimi sijafurahishwa na uamuzi uliofanywa na timu kumvua unahodha kulingana na kazi kubwa anayoifanya uwanjani lakini pia ingependeza zaidi kama wangemfanya nahodha msaidizi," alisema Shindika. Katika hatua nyingine Nahodha huyo wa zamani wa Taifa Stars mbali na kukumbushia jinsi yeye mwenyewe alivyovuliwa Unahodha wa...