Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 1, 2017

OMONG ALIANZA NA KIKOSI HIKI MECHI YAKE YA KWANZA

Picha
OMOG ALIANZA NA KIKOSI HIKI MECHI YAKE YA KWANZA, SIMBA IKILALA 1-0 VS ORLANDO HUKO SAUZ 1. Said Mohamed ‘Nduda’ 2. Ali Shomari  3. Jamal Mwambeleko  4. Salim Mbonde  5. Erasto Nyoni  6. Jonas Mkude 7. Jamal Mnyate 8. James Kotei 9. John Bocco  10. Emmanuel Okwi  11. Mohammed Ibrahim

SIMBA YAGONGWA KIMOKO BONDENI

Picha
VIGOGO wa soka Tanzania, Simba SC leo wame wamepoteza mchezo wao wa kwanza wa kujipima nguvu katika kambi yao ya Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya baada ya kufungwa 1-0 na wenyeji, Orlando Piates mjini Johannesburg. Kwa mujibu wa Msemaji wa Simba SC, Hajji Sunday Manara, Simba inayofundishwa na kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog ilicheza vizuri pamoja na kufungwa. Kipa mpya wa Simba, Aishi Manula (kulia) kutoka Azam FC akiwa kambini Afrika Kusini“Kwa mujibu wa maelezo ya benchi la Ufundi, mchezo ulikuwa mzuri na timu ilicheza vizuri, lakini bahati ilikuwa wenyeji Pirates kupata ushindi huo. Manara alisema Omog anayesaidiwa na Mganda, Jackson Mayanja aliwapa nafasi karibu wachezaji wote leo kucheza, akipanga vikosi viwili tofauti kila kipindi. Simba inatarajiwa kushuka tena dimbani Alhamisi kumenyana na mabingwa wa Afrika Kusini, Bidvest Wits kabla ya kurejea Dar es Salaam tayari kwa mchezo dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda Agosti 8, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ...

UTABIRI WA KIKOSI CHA YANGA

Picha
Bila kupepesa macho hiki ndio kitakuwa kikosi cha kwanza cha yanga msimu wa 2017-2018.... je wewe unaonaje...???

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 01.08.2017

Picha
TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 01.08.2017 Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28, hatojiunga na kikosi cha kwanza kwa ajili ya kuanza mazoezi siku ya Jumanne huku akiendelea kufuatilia uhamisho wake kuondoka Stamford Bridge. (Marca) Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri ameiambia Chelsea kuwa hawatomuuza beki wa kushoto Alex Sandro, 26. (Sport Mediaset) Meneja wa Chelsea Antonio Conte anataka kumsajili kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater, 27, baada ya Nemanja Matic kwenda Man Utd. (Mail) Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp huenda akaamua kumfuatilia kiungo wa Bayern Munich Renato Sanches, 19, iwapo Philippe Coutinho, 25, ataondoka kwenda Barcelona. (Bild) Bayern Munich wamekataa dau la pauni milioni 10 kutoka kwa AC Milan wanaomtaka Renato Sanches, 19, kwa mkopo. (Le10Sport) Beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26, atakuwa na mazungumzo na meneja wake mpya Mauricio Pellegrino, wiki hii, huku Liverpool wakijiandaa kuvunja rekodi yao ya usajili kumchukua beki huyo wa kimataifa ...

HARUNA NIYONZIMA RASMI SIMBA UTAKE USITAKE

Picha
Afisa Habari wa klabu ya Simba amethibitisha kwamba Haruna Niyonzima ni mchezaji halali wa klabu hiyo mara baada ya kumaliza mkataba na klabu yake ya zamani Yaga ambayo aliichezea hadi msimu uliopita. Kulikuwa na tetesi nyingi kuanzia kwenye vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na hata kwa wadau mbalimbali kuhusu Niyonzima kusainiwa na Simba lakini klabu hiyo haikuthibitisha mapema hilo. “Haruna Niyonzima ni mchezaji halali wa Simba tumeshamalizana nae, ameshamaliza mkataba na club aliyokuwa anaitumikia atakuja Simba. Anaweza akaenda South Africa kuungana na kikosi au anaweza kuja moja kwa moja Dar katika safari moja na Rayon Sport na atacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Rayon Sports siku ya Simba Day,” – Haji S. Manara Afisa Habari Simba SC. Yanga tayari walishatoa taarifa mapema kwamba hawakufikia makubaliano na Niyonzima baada ya star huyo wa Rwanda kutaka dau kubwa ili aongeze mkataba mpya wa kubaki Yanga. Kwa sasa Niyonzima yupo Rwanda mapumzikoni tangu kuma...

HARUNA NIYONZIMA RASMI SIMBA UTAKE USITAKE

Picha
Afisa Habari wa klabu ya Simba amethibitisha kwamba Haruna Niyonzima ni mchezaji halali wa klabu hiyo mara baada ya kumaliza mkataba na klabu yake ya zamani Yaga ambayo aliichezea hadi msimu uliopita. Kulikuwa na tetesi nyingi kuanzia kwenye vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na hata kwa wadau mbalimbali kuhusu Niyonzima kusainiwa na Simba lakini klabu hiyo haikuthibitisha mapema hilo. “Haruna Niyonzima ni mchezaji halali wa Simba tumeshamalizana nae, ameshamaliza mkataba na club aliyokuwa anaitumikia atakuja Simba. Anaweza akaenda South Africa kuungana na kikosi au anaweza kuja moja kwa moja Dar katika safari moja na Rayon Sport na atacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Rayon Sports siku ya Simba Day,” – Haji S. Manara Afisa Habari Simba SC. Yanga tayari walishatoa taarifa mapema kwamba hawakufikia makubaliano na Niyonzima baada ya star huyo wa Rwanda kutaka dau kubwa ili aongeze mkataba mpya wa kubaki Yanga. Kwa sasa Niyonzima yupo Rwanda mapumzikoni tangu kuma...

MWANARIADHA USAIN BOLT AFANANISHWA NA MUHAMMED ALI

Picha
Mwanariadha Usain Bolt afananishwa na Muhammed Ali Usain Bolt ana kipaji na ana ushawishi mkubwa miongoni mwa wanariadha kama Muhammed Ali alivyokuwa na ushawishi miongoni mwa mabondia, alisema Lord Coe. Bingwa huyo wa mbio fupi ambaye ameshinda medali ya dhabau katika michezo ya olimpiki mara nane anatarajiwa kustaafu baada ya mashindano ya ubingwa mjini London, yalioanza siku ya Ijumaa. Coe alimfananisha raia huyo wa jamaica na mmoja wa wanamichezo mashauri duniani Muhammed Ali. Ni bingwa wa mbio fupi duniani, alisema Coe ambaye ndiye rais wa Shirikisho la Wanariadha Duniani (IAAF). "Usain Bolt ana kipaji, Siwezi kumfananisha na mwanamichezo mwingine yeyote yule zaidi ya Muhammad Ali ambaye amekuwa na ushawishi mkubwa nje na ndani ya michezo." Unaweza kuanzisha mjadala kuhusu ni nani mchezaji bora wa soka duniani ama mchezaji wa tenis bora, lakini hakuna mjadala kuhusu Bolt katika mbio fupi. Mwanariadha huyo wa Jamaica alishinda mbio za mita 100, 200 na 4 mara 100 k...

WACHEZAJI WASIOPIMWA AFYA KUTOSHIRIKI LIGI MSIMU UJAO

Picha
Wachezaji wasiopimwa afya kutoshiriki ligi msimu ujao Wachezaji ambao hawatathibitishwa afya zao hawataruhusiwa kucheza katika ligi kuu Tanzania Bara, ligi daraja la kwanza pamoja na ligi daraja la kwanza msimu ujao wa 2017/18 Katazo hilo ni kwa mujibu wa mabadiliko ya kanuni za ligi hiyo yaliyofanywa na kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika kikao chake cha Julai 30 mwaka huu, ambacho pia kilipitisha mambo mbalimbali. Katika mabadiliko hayo, mchezaji atakayesajiliwa hatapewa leseni ya kumruhusu kucheza mashindano husika kama hatakamilisha masharti makuu matatu. Masharti hayo ni kukatiwa bima ya matibabu, kuidhinishwa afya yake ambapo fomu yake itapaswa kupitishwa na kamati ya tiba ya TFF na sharti la tatu ni kuwasilisha TFF mkataba wake wa maandishi 'hardcopy'. Kuhusu suala la mikataba, kanuni ya 69 (8), imeendelea kusisitiza kwamba: "Mikataba yote ya wachezaji ambayo haijasajiliwa na kuthibitishwa na TFF, haitatambuliwa” Kaimu Rais wa TFF, ...

ZIMBWE JR. ANUNUA VIATU MAALUMA KWA NGOMA

Picha
Beki ambaye pia ni Nahodha Msaidizi wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ atakaporudi Bongo atakuwa na kiatu cha kuchezea mpira chenye thamani ya Sh700,000. Tshabalala ambaye alikuwa mapumzikoni akijiuguza mguu, amerudi uwanjani kwa kasi na sasa anataka atakapoanza kuonekana akamilike. Alipofika hapa Afrika Kusini, akafanya kweli akatoa kiasi cha Rand 3,500 ambazo ni kama laki saba za Kibongo na kununua kiatu hicho. Tshabalala ataonekana na kiatu hicho ambacho ni Nike ya kupanda kinachoonekana kama kimeungwa na soksi. Amepanga kukivaa katika mchezo wao wa kwanza wa Simba Day na ule wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga. “Kazi yangu mpira, lazima niupe heshima na ndiyo maana hata kununua kiatu hiki sikuona uchungu, ningekuwa msanii ndiyo ningehangaika na mavazi na cheni, lakini mimi ni mchezaji,” alisema

OKWI AINGIA MKATABA NA OMONG

Picha
HAPA Afrika Kusini mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi anavaa jezi namba saba huku ile namba 25 ikiendelea kuvaliwa na Shiza Kichuya na ameliambia benchi la ufundi kwamba amerudi Msimbazi kwa ajili ya kufanya kazi na wanaobisha wataona. Okwi ambaye baada ya kuwasili Afrika Kusini alikaa na kocha wake, Mcameroon Joseph Omog kwa masaa machache na kuzungumza. “Ninajivunia kuwa na mchezaji kama Okwi ndani ya timu kwa sababu kila mmoja anamfahamu, kipindi kile sikumwona akicheza ligi lakini sifa zake na ninavyomwona kwenye video sina wasiwasi,”alisema Omog ambaye awapo mazoezini amekuwa na msimamo na mkali kuhakikisha kazi inafanyika. “Alipofika nimekaa na kuzungumza naye kwa masaa kadhaa, ana nidhamu na ameniahidi kufanya kazi ya maana sana na tumekubaliana jambo ambalo limefurahisha kutokana na mipango yake, ni mchezaji mkubwa anayejitambua, nasubiri kazi.” Hata hivyo, licha ya Okwi kufanyia mazoezi jezi namba saba, huenda mchezaji huyo akarudishiwa jezi yake n...