Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 3, 2017

PSG KUHOJIWA NA FIFA JUU YA FEDHA ZA KUMNUNUA NEYMA JR.

Picha
Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) limepanga kuihoji klabu ya PSG ilikozitoa fedha ambazo zitatumika kumsajili nyota wa Barcelona, Neymar Jr. Kiwango hicho cha fedha kimelishtua shirikisho hilo ikiwa ni fedha ya usajili ambayo inatarajiwa kuvunja rekodi ya dunia kwa kumsajiri mchezaji mmoja. Shirikisho hilo limesema kwamba halitasita kuiadhibu klabu hiyo ya Ligue 1 iwapo litabaini kukiuka kanuni za usajili kwa wachezaji.

YANGA WAIBEBESHA LAWAMA TFF, VODACOM, WADAI HAWAKUALIKWA

Picha
Yanga waibebesha lawama TFF, Vodacom, wadai hawakualikwa 03 Aug 2017, 08:14 pm| By Wingiasa SOKA TANZANIA                        Uongozi wa Yanga umeonyesha kutofurahishwa na kitendo cha kutoalikwa katika hafla ya ukabidhi wa vifaa iliyofanywa na wadhamini wa Ligi Kuu Bara, kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom.   Wakati wa kukabidhiwa jezi hizo,  Yanga haikuwa na mwakilishi na badala yake, Msemaji wa Simba, Haji Manara akafanya “uchale”, kwenda kuwa sehemu ya mwakilishi wa Yanga wakati vijana husika wakionyesha jezi za Yanga za msimu ujao, jukwaani.   Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa akizungumzia hilo amesema wamesikitishwa na jambo hilo na hasa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Tanzania, wameonekana kutowatendea haki.   "Hicho kitendo kimetusikitisha sana, kiuweli hali hiyo inatufanya tuonekane wazembe kwa mashabiki wetu kutokana na TFF ambao ndiyo waratibu...

MSIMU MPYA WA LIGI KUU YA VODACOM TAZANIA BARA WAZINDULIWA LEO

Picha
MSIMU MPYA WA LIGI KUU YA VODACOM WAZINDULIWA LEO DAR  DAR ES SALAAM MSIMU mpya wa Ligi Kuu ya soka ya Vodacom Tanzania Bara umezinduliwa rasmi leo kwa wadhamini wakuu, kampuni ya Vodacom Tanzania kukabidhi vifaa kwa timu zote 16 zitakazoshiriki ligi hiyo msimu ujao. Zoezi hilo limefanyika mjini Dar es Salaam leo na Vodacom wanaodhamini Ligi Kuu inayorushwa moja kwa moja na Azam TV, wamekabidhi vifaa mbalimbali zikiwemo jezi, viatu, mipira na suti za kimichezo. Akikabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi wa Idara ya Masoko ya Vodacom, Hisham Hendi amesema kwamba, kwa mara nyingine tena katika kuhakikisha Ligi Kuu ya soka hapa nchini inaenda vizuri wanakabidhi vifaa vya ubora wa hali ya juu. Msemaji wa Simba SC, Hajji Sunday Manara (katikati) akisalimiana na vijana waliokuwa wanaonyesha jezi za Yanga katika uzinduzi huo Hajji Manara akiwa katikati ya vijana walioonyesha jezi za Simba Viongozi wa Vodacom, Bodi ya Ligi na klabu zote 16 za Ligi Kuu wakiwa katika picha ya pamoja Hendi...

ERASTO NYONI AIBEBA SIMBA DHIDI YA BIDVET

Picha
Jo'burg, Afrika Kusini. Mabingwa wa Kombe la FA, Simba imelazimisha sare ya bao 1-1 na Bidvest Wits katika mchezo wake wa pili wa kirafiki uliofanyika leo Afrika Kusini. Katika mchezo bao pekee la Simba lilifungwa na beki mpya wa timu hiyo Erasto Nyoni katika dakika 32. Matokeo hayo ni faraja kwa Simba inayojiandaa na mchezo wa Ngao wa Jamii dhidi ya Yanga baada ya kupokea kichapo katika mechi ya kwanza kwa bao 1-0 kutoka kwa Orlando Pirates. Kikosi kilichoanza Simba ni. Aishi Manula, Erasto Nyoni, Jamal Mwambeleko, Salim Mbonde, Method Mwanjali, James Kotei, Jamal Mnyate, Mdhamiru Yassin, John Bocco, Emmanuel Okwi, Mohamed Ibrahim.

SINGIDA UNITED YAJAA MINOTI

Picha
Dar es Salaam. Klabu ya Singida United imepata mdhamini mpya kampuni ya YARA Tanzania wameingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya zaidi ya Sh 250 milioni. Yara ni kampuni ya Norway inayojishughulisha na masuala ya kilimo sasa watakuwa mdhamini Singida United pamoja na Sportpesa, kampuni ya mafuta ya Puma. Akizungumza wakati wa hafla ya kusainishana mkataba huo iliyofanyika ukumbi wa hoteli ya Serena jijinj Dar es Salaam, Mkurugenzi mtendaji wa YARA, Alexandre Macedo alisema wameamua kuingia Singida United baada ya kuona klabu hiyo ina nembo ya mafuta ya alizeti. "Tunashughulika na kilimo, Singida United tuliona ni klabu inayojihusisha na kilimo cha mafuta ya kula, hivyo tumeona ni vyema kushirikiana nao maana hii ni ajira kwa vijana," alisema Macedo. Mkurugenzi wa klabu hiyo, Festo Sanga aliishukuru YARA na kuahidi kushirikiana nao ikiwa ni pamoja na kuitangaza. “Tuliomba udhamini kwao na hawakusita kwani tayari tumepata ekari zaidi ya 100 ambazo tutalima kwa kushi...