Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 9, 2017

KAULI YA NIYONZIMA LEO HII MAZOEZINI

Picha
“Najua kuna chuki na maneno ya kejeli yameanza kusemwa juu yangu lakini mimi sijali, ninachowaza ni namna gani naweza kuipa timu yangu mafanikio kwa sababu ndiyo inayoniweka hapa Tanzania na nitajibu maneno yao kwa kutumia miguu yangu na siyo mdomo,”- Haruna Niyonzima Toa maoni yako

SIMON MSUVA KUTUA HISPANIA KWA SIKU SABA

Picha
Dar es Salaam. Winga wa Mtanzania, Simon Msuva amesafiri na kikosi cha timu yake ya Difaâ Hassani El Jadidi kwenda nchini Hispania kuweka kambi ya siku saba. Katika kambi hiyo watakuwa na michezo kadhaa ya kujima ubavu kabla ya kurejea Morocco kwa ajili ya kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu nchini humo 'Batola Pro'. Msuva amesajili na klabu hiyo ya Morocco akitokea Yanga ambayo aliitumikia msimu uliopita.

NIYONZIMA AAHIDI ZAWADI KWA KAZIMOTO

Picha
Niyonzima aahidi zawadi kwa Kazimoto Nyota mpya wa Simba aliyesajiliwa hivi karibuni baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga, Haruna Niyonzima ameahidi kumtafutia zawadi kiungo mkongwe wa klabu hiyo, Mwinyi Kazimoto kutokana na hatua yake ya ‘kumvulia jezi. Kazimoto aliyekuwa akivaa jezi namba 8, ameamua kumuachia kiungo huyo raia wa Rwanda baada ya kuombwa kufanya hivyo kama ishara ya heshima kwake. “Namshukuru sana Mwinyi kwa heshima aliyonipa, na mimi namuahidi kumtafutia zawadi, ni lazima nimzawadie kwa hili alilonifanyia” amesema Haruna Akizungumzia sababu za kuiomba jezi hiyo, Haruna ambaye mara nyingi hucheza kama kiungo namba 8, amesema jezi hiyo ina kumbukumbu kubwa katika maisha yake ya soka, na ndiyo aliyokuwa akiivaa wakati akiwa Yanga Niyonzima ambaye ameanza kuonyesha cheche katika klabu ya Simba kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Rayon Sports iliyopigwa jana kuadhimisha Simba Day, ameahidi kuitumikia Simba kwa nguvu zote katika mechi zote na amesema ataanza na m...

LWANDAMINA AJIPIGA KIFUA JUU YA KIKOSI CHAKE

Picha
Kocha mkuu wa Yanga, Mzambia George Lwandamina ameanza kulidhishwa na maandalizi ya timu yake kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Kikosi hicho cha Lwandamina kitakuwa na kibarua kizito cha kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Bara kuanzia Agosti 27 itakapocheza dhidi ya Lipuli kwenye Uwanja wa Taifa. Yanga ilianza maandalizi ya msimu mpya kwa kufanya mazoezi ya Gym jijini hapa kabla ya kwenda mkoani Morogoro ambapo waliendelea na mazoezi ya kujenga utimamu wa mwili kwa kukimbia na mapalashuti. "Tumejiandaa na tunaweza kuanza ligi, ni wazi kuwa msimu huu utakuwa na ushindani mkubwa kwa sababu timu nyingi zimejiandaa na hata kusajili vizuri," alisema Lwandamina. Katika mazoezi ya leo asubuhi kwenye Uwanja wa Polisi Kurasini, kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa alikuwa akitilia mkazo namna ya ukabaji. Yanga inajiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba utakaofanyika Agosti 23, jambo lililomfanya Nsajingwa kuwa mkali kwa makosa ya kizembe yaliyokuwa yaki...

PSG WAMNYAPIA ALEXIS SANCHEZ

Picha
Arsene Wenger ameelezea mstari ambao Alexis Sanchez hauzi kuuzwa wakati wa majira ya joto, lakini Ripoti ya Independent ya kwamba Paris Saint-Germain itafanya hoja kubwa zaidi ya £ 80 milioni, wiki tu baada ya kupiga rekodi ya dunia kwa £ 200,000 Senda kwa Neymar. Vigogo vya Ligue 1 vinabaki kwenye soko kwa mshambuliaji na wanaendelea kufuatilia Kylian Mbappe, lakini Sanchez bado ni lengo la juu. Chile inaaminika kuwa tayari kukaa baada ya uamuzi wa Gunners kumsimamia, licha ya mwaka mmoja tu iliyobaki kwenye mpango wake. Baada ya kugonga tena mpango mpya wa thamani ya £ 250,000 kwa wiki ili kupanua kukaa kwake kwa Emirates, PSG itatoa £ 400,000 kwa wiki kwa jitihada za kumshawishi Sanchez kuwachagua juu ya Manchester City. Lakini tamaa ya Sanchez ya kufanya kazi na Pep Guardiola ni kwamba mji huo unaaminika kuwa unaweza kukubaliana na masharti ya mkataba mpya wa mkataba wa Gunners.

OBREY CHIRWA AMESHAIVA KIBONGO

Picha
Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa ameanza kuiva bana katika uzungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Chirwa anaweza kufanya mawasiliano na wachezaji wenzake kwa Kiswahili japo anaongea kama mtu mwenye kigugumizi katika utamkaji wa maneno lakini anaonekana kuanza kukifahamu vizuri. Kuna muda staa huyo wa Yanga huwa anachanganya maneno pale anaposhindwa kutumia neno fasaha la Kiswahili. Mzambia huyo amedai kuwa karibu na wachezaji wenzake, kumemfanya kukifahamu Kiswahili kwa haraka. "Muda mwingi huwa nasikia Kiswahili kikizungumuzwa na wachezaji wenzangu huwa najifunza, sio kwamba hii ni lugha ni ngumu hapana,"alisema Chirwa.

BALOTELLI APATA MSALA MWENGINE

Picha
Unaweza ukasema, yaleyake. Mario Balotelli hakui maana kila siku, vituko tu. Safari ameng’ang’aniwa na Polisi baada ya kuendesha gari lake mwendo kasi kupitiliza hadi kufikia mail 125 kwa saa. Balotelli alikuwa akiendesha gari aina ya  Ferrari, amekamatw ana Polisi nchini Italia. Mshambuliaji huyo wa Nice ya Ufaransa, alikuwa akikimbia kwa kasi hiyo huku akijua hairuhusiwi kufanya hivyo. Polisi hao waliokuwa katika eneo la Vicenza walifanikiwa kumkimbiza na kumsimamisha kabla ya baadaye kumkamata. Moja ya faini aliyopigwa ni kwa kuwa gari lake limesajiliwa mwendo mkubwa kuwa ni maili 105 kwa saa na si zaidi.

AZAM WATAMBA KUREJESHA MAKALI WAKIRUDI UGANDA

Picha
KIKOSI CHA AZAM FC MSIMU ULIOPITA Kocha Mkuu wa kikosi cha Azam, Aristica Cioaba raia wa Romania ameweka wazi kuwa makali ya kikosi chake hicho yataongezeka baada ya kurejea nchini wakitokea Uganda ambapo wameenda kuweka kambi. Azam wamekimbilia nchini Uganda kuweka kambi ya wiki mbili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi utakaoanza Agosti 26, mwaka huu ambapo wakiwa huko watacheza mechi za kirafiki na timu za KCCA, Vipers, URA na Onduparaka. Mromania huyo amesema kuwa kambi hiyo ya nje ya Tanzania waliyoipata itakiwezesha kikosi chake kujinoa kwa utulivu na kuwasaidia nyota wake kuungana kwa pamoja na kutambuana wanavyocheza, jambo ambalo litasaidia kutimiza kile ambacho anakitaka kwenye msimu ujao. “Kambi ya huku Uganda ina faida kubwa kwetu, na labda nikuhakikishie kuwa tukitoka huko tutakuwa moto wa kuotea mbali kwenye ligi kuu kwani wachezaji wangu watakuwa wameshika kile nitakachowafundisha kwa kiasi kikubwa. “Unajua mnapokuwa nje mnapata nafasi ya kuwa huru ku...

KIUNGO WA YANGA TSHISHIMBI ANAKABA HADI KIVULI

Picha
      4 hrs ago    Michezo ,  Yanga Kiungo mpya wa Yanga, Kabamba Tshishimbi ameonyesha uwezo mkubwa wa kukaba na kuanzisha mashambulizi kwa haraka katika mazoezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Polisi Kurasini, Dar es Salaam. Yanga ilikuwa na mazoezi ya kuchezea mpira kwa kugawana vikosi vitatu ambapo katika mazoezi hayo kiungo huyo aliyesajiliwa kutoka Mbambane Swallows alionekana kutakata. Akizungumza baada ya kumaliza mazoezi hayo Tshishimbi amesema kuwa lengo lake ni kushinda mataji akiwa na Yanga. "Napenda kuwa mshindi siku zote, nimekuja Tanzania kushinda mataji nikiwa na Yanga hivyo nitajitahidi kuisaidia timu kwa uwezo wangu wote," alisema Tshishimbi. Naye  Andrew Vicent " Dante alimuongelea kiungo huyo na kusema ni moja ya wachezaji wazuri waliosajiliwa kipindi hiki cha usajili. "Jamaa yupo fiti siyo mwepesi kwa maana ya kuchukua mpira mguuni kwake,  kikubwa ni kushirikiana naye vizuri  maana bado anahitaji muda wa kuendana na...

MASHABIKI SIMBA WAFUNIKA SIMBA DAY

Picha
Dar es Salaam . Mashabiki wa Simba wamejitokeza kwa wingi kushuhudia tamasha la klabu yao la Simba Day. Twende kisport iliwasili Uwanjani hapo saa 1: 5 1 na kushuhudua misururu ya mashabiki wengi wakisubiri kuingia uwanjani. Ndani ya uwanjani kulishuhudia majukwaa ya mashabiki wa Simba yakiwa yamejaa kufikia saa 8:02 huku mashabiki wakihamia majukwaa ambayo hukaliwa na mashabiki wa Simba. "Usajili uliofanywa na viongozi unatupa imani kubwa ya kufanya vizuri. Natka kushudia wachezaji wapya kwakuwa nimekuwa nikiwasikia tu kwenye magazeti,"alisema Kudra Musa.

MANARA SASA ILE SIFA

Picha
Ofisa Habari wa Simba Haji Manara haishiwi vituko pale anapotekeleza majukumu ya klabu yake. Ni hivi. Wakati mashabiki wa Simba wakijiuliza viongozi wao wako wapi hawaonekani uwanjani, Haji aliibuka na kuzua shangwe kwa wanazi wengi wa klabu hiyo waliofika Uwanja wa Taifa. Haji alibebwa mkukumkuku na wanenguaji wa kundi la Msondo Ngoma na kujumuika nao kulisakata rumba. "Pamoja na Aveva na Kaburu kuwa mahabusu lakini tukio hili limefana sana, ni dhahiri matumaini yetu mashabiki wa Simba ni kutisha kimataifa,"alisema Hamis Seif, shabiki wa S imba

NIYONZIMA NA OKWI WAFUNIKA TAIFA

Picha
Uwanja wa Taifa ulisimama kwa muda wakati wachezaji wawili wa Simba, Emanuel Okwi na Haruna Niyonzima wakutambulishwa. Viongozi mbalimbali waliokuwemo jukwaa kuu pia hawakusita kupiga makofi wakati Niyonzima na Okwi wakitambulishwa. Waziri wa Mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba ambaye ni shabiki wa kugalagala wa Yanga alishindwa kuzuia hisia zake baada ya Niyonzima na Okwi kutambulishwaa. Okwi na Niyonzima waliwahi kuichezea Yanga na msimu huu wamekuwa gumzo baada ya kununuliwa na Simba. Wakati huo huo; Kiungo wa Simba, Mwinyi Kazimoto ameridhia kumkabidhi jezi namba 8 kiungo mpya Niyonzima. Niyonzima amesajiliwa kuitumikia Simba msimu hu baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga. "Limetokea jambo kubwa kambini, Kazimoto ameridhia kumpa jezi Niyonzima," amesema Haji Manara kabla ya kuanza kuwatambulisha wachezaji wa timu hiyo

THIS IS SIMBA BROTHER

Picha
Dar es Salaam. Bao la kiungo Mohamed Ibrahimu limetosha kuipamba Simba Day kwa wenyeji Simba kushinda bao1-0 dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda kwenye Uwanja wa Taifa. Ushindi huo umekuwa ni faraja kubwa kwa mashabiki wa Simba waliofuriki uwanjani hapo wakati wa kushudia wachezaji wao wapya wakitambuliwa. Kiungo Mo Ibrahimu aliwainua mashabiki wa Simba katika dakika ya 16, akimalizia pasi ya Emmanuel Okwi. Bao hilo lilitokana na pasi fupi walizopigiana James Kotei, Muzamiru Yassin na Okwi kabla ya kuupeleka mpira kwa Ibrahim aliyepiga shuti la chini chini lililomshinda kipa wa Rayon na kujaa wavuni. Viungo washambuliaji wa Simba waliocheza nyuma ya John Bocco walicheza kwa maelewano mazuri ya uchezaji kuanzia kwenye namna ya kubadilishana nafasi mara kadhaa Okwi amekuwa akihama upande wa kushoto na kuja kucheza nyuma ya Bocco wakati huo Ibrahimu naye akienda upande aliotoka Okwi vivyo hivyo na upande wa Kichuya na kuwapa wakati mgumu mabeki wa Rayon katika kuwazuia. Pamoja na bao hil...