SIMBA SPORTS DAR ES SALAAM 11-8-2017 TAARIFA KWA UMMA _______________________________ Klabu ya Simba inawatangazia Wanachama wake na wadau wa mchezo wa kandanda kote nchini kuwa Mkutano wake mkuu wa kawaida wa kila mwaka upo pale pale. Hatua hiyo inafuatia na Hukumu iliyosomwa leo katika Mahakama ya kisutu, kufuatia zuio la kuzuia Mkutano huo, liliowekwa na mmoja wa wadhamini wa klabu Mzee Hamis kilomoni. Kwenye hukumu hiyo,mahakama hiyo ilitupilia mbali shauri hilo. Mkutano huo utafanyika siku ya Jumapili tarehe 13-8-2017, kuanzia saa Nne kamili asubuhi, ukitanguliwa kwa Wanachama wa klabu kujiandikisha kuanzia saa mbili kamili asubuhi. Klabu imeamua kufanyia mkutano huo kwenye Ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyarere international Conference Centre). Ukumbi huo wa kisasa kabisa nchini upo maeneo ya Ocean Road, jirani na Chuo c...