Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 23, 2017

SIMBA YATWAA NGAO YA JAMII KWA MATUTA

Picha
Dar es Salaam. Kipa Aishi Manura na kiungo Mohamed Ibrahimu wameiongoza Simba kutwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii kwa kuifunga Yanga kwa penalti 5-4. Katika mchezo huo uliomalizika dakika 90 kwa timu hizo kutoka suluhu ndipo penalti zilipotumika kuamua bingwa wa mechi hiyo ya ufunguzi wa msimu mpya wa 2017-18. Kipa Manura aliyesajili na Simba akitokea Azam alithibisha ubora kwa kudaka penalti ya kwanza ya Yanga iliyopigwa na Kelvin Yondani. Wakati Mo Ibrahimu alifungia Simba penalti ya sita baada ya kiungo wa Yanga, Juma Mahadhi kuikosa penalti yake ya sita kwa kupaisha. Wafungaji wa Simba katika penalti hizo ni nahodha Method Mwanjali, Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima, Shiza Kichuya wakati Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ akikosa kabla ya Mo Ibrahimu kufunga penalti ya sita. Yanga ilianza penalti hizo vibaya kwa Kelvin Yondani na baadaye Juma Mahadhi kukosa huku walipopata ni nahodha Thaban Kamusoko, Pappy Tshishimbi, Ibrahimu Ajib, Donald Ngoma. Simba ilianza mechi hiyo kwa k...

KIKUKU CHA TSHISHIMBI CHAWA GUMZO

Picha
Kiungo mpya wa Yanga, Pappy Tshishimbi amezua minong’ono kwa mashabiki wa soka kutokana na kufunga cheni ‘kikuku’ katika mguu wake wa kushoto. Tshishimbi aliwaduwaza mashabiki wakati aliposhikuka kwenye basi la Yanga akiwa na wachezaji wenzake na kuingia uwanjani tayari kuivaa Simba. Kiungo huyo Mkongo alichelewa kujiunga na Yanga kutokana na matatizo yake ya kupata viza, hata kibari chake cha kuanza kuichezea Yanga kilipatikana leo asubuhi.