JAMHURI KIHWELO "JULIO" ASHANGAA MAKOCHA WATANZANIA KUTOAMINIWA STARS

Kocha wa zamani wa klabu ya Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio' ameshangaa kutokuona watanzania wakipewa nafasi ya kuifundisha Taifa Stars.

Kauli ya Julio imekuja siku chache mara baada ya Kocha Mrundi Ettiene Ndayiragije kuchaguliwa kukaimu nafasi ya Emmanuel Amunike aliyekuwa akiinoa timu hiyo.

Julio amemtaja Abdallah King Kibadeni kuwa mmoja wa makocha ambao wana heshima kuwa katika soka la Tanzania akipendelea wapewe nafasi hiyo.

Kocha huyo mwenye maneno mengi anaamini Kibadeni ambaye aliwahi kuinoa na kuichezea Simba pia anafaa kuinoa Stars kwa heshima aliyoiweka Tanzania .

"Nashangaa kwanini wazawa hawapewi nafasi.

"Tuna watu wengi ikiwemo King Kibadeni ambaye anaweza akachukua nafasi hiyo na akaifundisha Stars." @by wingi van moses jr

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MBARAKA YUSUPH BADO HALI TETE

NIYONZIMA AAHIDI ZAWADI KWA KAZIMOTO