Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 17, 2019

WACHEZAJIWA SIMBA WALIOBAKI DSM KWENDA BONDENI MDA WOWOTE

Picha
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Simba Sc zinasema Nyota wanne wa klabu hiyo ambao waliachwa jiji Dar Es Salaam wakati wenzao wakielekea Afrika Kusini kwenye maandalizi ya msimu mpya tayari wamekamilisha masuala ya Passport zao na muda wowote watasafiri kuwafuata wachezaji wengine. . . Nyota hao ni pamoja na Meddie Kagere, Deo Kanda, Francis Kahata na Sharaf Eldin Shoboub

AZAM KANYAGA TWENDE KAGAME CUP

Picha
MABINGWA watetezi, Azam FC wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) leo Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali, Rwanda. Haukuwa ushindi mwepesi, kwani Azam FC ililazimika kutoka nyuma ili kupata tiketi ya Nusu Fainali, baada ya kutanguliwa kwa bao la Ipamy Giovanni dakika ya 21. Mshambuliaji mpya, Iddi Suleiman ‘Nado’ aliyesajiliwa kutoka Mbeya City alianza kuisawazishia Azam FC dakika ya 27 akimalizia mpira uliorudi baada ya kuokolewa kwa kichwa kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Mzimbabwe, Bruce Kangwa kutoka kushoto. Wachezaji wa Azam FC wakimpongeza Obrey Chirwa baada ya kufunga bao la ushindi wa 2-1 dhidi ya TP Mazembe Na alikuwa Iddi Nado mwenyewe aliyesababisha faulo hiyo baada ya kuangushwa na Giovanni pembezoni mwa Uwanja kabla ya beki wa kimataifa wa Zimbabwe kwenda faulo iliyozaa bao lililoirejesha Azam mchezoni. Na sifa zimuendee...

MZEE KILOMONI APIGWA CHINI MSIMBAZI

Picha
Hizi ni barua zilizotoka kwa Kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali kwenda kwa wakili wa aliyekuwa mdhamini wetu, na pia barua ya Mahakama kwenda kwa wakili huyo zinazothibitisha mdhamini huyo Mzee Hamis Kilomoni sio mdhamini tena wa klabu yetu ya Simba. Taarifa hii ilitolewa leo na Afisa Mtendaji Mkuu, Crescentius Magori kwenye mkutano wake na wanahabari.

ABDI BANDA ANOGESHA KAMBI YA SIMBA UKO BONDENI

Picha
BEKI wa zamani wa Simba ambaye kwa sasa anakipiga timu ya FC Baroka ya Afrika Kusini leo amekutana na wachezaji wa Simba pamoja na viongozi ambao wametua timu Afrika Kusini kuweka kambi. Beki huyo ameongeza furaha kwa wachezaji na viongozi wa Simba baada ya kuonana na kupiga picha ya kumbukumbu Simba imeamua kuweka kambi ya muda wa wiki mbili nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao unaotarajiwa kuanza Agosti 23 na mchezo wa kwanza itamenyana na JKT Tanzania. @Wingi van moses jr.

JAMHURI KIHWELO "JULIO" ASHANGAA MAKOCHA WATANZANIA KUTOAMINIWA STARS

Picha
Kocha wa zamani wa klabu ya Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio' ameshangaa kutokuona watanzania wakipewa nafasi ya kuifundisha Taifa Stars. Kauli ya Julio imekuja siku chache mara baada ya Kocha Mrundi Ettiene Ndayiragije kuchaguliwa kukaimu nafasi ya Emmanuel Amunike aliyekuwa akiinoa timu hiyo. Julio amemtaja Abdallah King Kibadeni kuwa mmoja wa makocha ambao wana heshima kuwa katika soka la Tanzania akipendelea wapewe nafasi hiyo. Kocha huyo mwenye maneno mengi anaamini Kibadeni ambaye aliwahi kuinoa na kuichezea Simba pia anafaa kuinoa Stars kwa heshima aliyoiweka Tanzania . "Nashangaa kwanini wazawa hawapewi nafasi. "Tuna watu wengi ikiwemo King Kibadeni ambaye anaweza akachukua nafasi hiyo na akaifundisha Stars." @by wingi van moses jr