Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 18, 2019

IBRAHIM AJIBU AKIONA CHA MOTO

Picha
AKIWA Rustenburg, Afrika Kusini kiungo mshambuliaji mpya wa Simba, Ibrahim Ajibu na Francis Kahata wamekiona cha moto ni baada ya Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems kutumia saa mbili sawa na dakika 120 kuwakimbiza nyota hao. Hiyo, ikiwa ni saa chache tangu timu hiyo itue Sauzi na kuweka kambi kwenye moja ya hoteli nyota tano ya Royal Marang Hotel ya nchini huko ikijiwinda na Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Bara. Ajibu alijiunga na Simba hivi karibuni akitokea Simba mara baada ya mkataba wake kumalizika wa kuichezea timu hiyo huku Kahata yeye amejiunga na timu hiyo baada ya mkataba kumalizika Gor Mahia ya nchini Kenya. Ibrahim Ajibu atakaa siku sita tu katika kambi yao ya Afrika Kusini kisha atarejea hapa na kujiunga na Taifa Stars. Meneja wa timu hiyo Patrick Rweyemamu alisema mara baada ya kutua huko juzi Jumatatu walifanya program moja ya mazoezi ya jioni kwa kutoa uchovu wa safari lakini siku iliyofuata walifanya mara mbili asubuhi na jioni. Rweyemamu alisema, programu waliyoanza...

CAF YAFANYA MABADILIKO

Picha
Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF, limetoa mwongozo mpya kuelekea michuano ya Klabu Bingwa Afrika CAFCL msimu ujao. Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya vilabu Afrika CAF imesema kuwa katika michezo ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika CAFCL na Kombe la Shirikisho CAFCC, utapigwa mchezo mmoja pekee badala ya michezo miwili. Pia mchezo huo mmoja utapigwa katika katika uwanja huru hauna uhusiano na timu yoyote kati ya zilizoingia fainali. Mabadiliko hayo yamekuja kufuatia kuzuka kwa sintofahamu katika mchezo wa pili wa fainali ya Klabu Bingwa Afrika msimu uliopita kati ya Wydad Casablanca na Esperance de Tunis, ambao haukumalizika kwa utaratibu licha ya Wydad kutangazwa mshindi na kukabidhiwa kombe na baadaye kupokonywa. Mwongozo huo mpya utazigusa timu wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Simba SC na Yanga zitakazoshiriki Klabu Bingwa Afrika, pamoja na Azam FC na KMC ambazo zitashiriki Kombe la Shirikisho endapo zitaweza kufika hatua ya fainali.