JEREMIA KISUBI AOMBA KUONDOKA SIMBA

CONFIRMED!! Golikipa wa Klabu ya Simba SC,Jeremiah Kisubi ameomba kuondoka kwa mkopo ndani ya Klabu hiyo kwenye Dirisha dogo la Usajili litakalofunguliwa Disemba 15 Mara baada ya kushindwa kupenya kwenye Kikosi Cha Kwanza Cha Simba na kuishia kuwa chaguo namba tatu. Kisubi ameomba kurejeshwa kwenye Klabu yake ya zamani ya Tanzania Prisons ambapo waajiri wake hao wa zamani wamemwambia kuwa wapo tayari kumlipa Mshahara robo ya ule anaopokea Simba SC kwa mda wote wa mkopo na robo tatu inayobaki wamlipe Simba. Bado hawajafikia maridhiano Kati ya Simba na Tanzania Prisons na Kila kitu kikikaa sawa Kisubi ataonekana tena Prisons kuanzia Dirisha dogo litakapofunguliwa. #wingi_van_mosesUpdates