TFF KUZIPUNGUZIA MZIGO SIMBA NA YANGA

Dar es Salaam. Kamati ya utendaji ya shirikisho la soka Tanzania (TFF), imezipunguzia mzigo za Ligi Kuu baada ya kuridhia kupunguza ada inayolipwa kwa wachezaji wa kigeni wanaosajiliwa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF leo, kila mchezaji wa kigeni anayesajiliwa na klabu inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara sasa atalipiwa ada ya Shilingi milioni mbili tofauti na hapo awali ambapo kanuni ilitaka kila mchezaji wa kigeni alipiwe ada ya Dola 2000 (Sh.4.5 milioni). Mabadiliko mengine ya kanuni ambayo kamati ya utendaji ya TFF imeyaridhia ni kutotambuliwa kwa mkataba wa mchezaji ambao haujasajiliwa na shirikisho hilo sambamba na wachezaji kukatiwa bima za afya. Masharti hayo ni kukatiwa Bima ya Matibabu, Kuidhinishwa afya yake ambayo mara baada ya fomu yake kupitishwa na Kamati ya Tiba ya TFF kwa mujibu wa Kanuni ya 18 (1) ya Ligi Kuu na Mkataba wake wa maandishi ‘hardcopy’ kuwasilisha TFF kwa mujibu wa Kanuni ya 69 (8) ya Ligi Kuu. Kama kuna timu haitakidhi japo sharti ...