ARSENAL YAITIA NIASHAI CHELSEA NGAO YA JAMII
Arsenal yaitoa nishai Chelsea ngao ya jamii Arsenal wamefanikiwa kutwaa ngao ya jamii kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza (EPL) kwa kuwafunga mabingwa wa ligi hiyo msimu ulipita, timu ya Chelsea. Washika mtutu hao wa London ambao ni mabingwa wa kombe la FA, (Ubingwa walioupata kwa kuwafunga hao hao Chelsea), leo wamenyakua ngao hiyo kwa mikwaju ya penati 4-1 baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya goli moja kwa moja. Katika mchezo huo Chelsea walitangulia kupata bao kupitia kwa Victor Moses dakika ya 46 ya mchezo, kabla ya Sead Kolasinac kusawazisha dakika ya 82. Katika mikwaju ya penati, Arsenal walifunga penati nne kupitia kwa Walcott, Nacho, Chamberlain na Giroud na kwa upande wa Chelsea, Morata na Courtois walikosa penati zao huku Garry Cahili akifunga penati yake