IBRAHIM AJIBU AKIONA CHA MOTO

AKIWA Rustenburg, Afrika Kusini kiungo mshambuliaji mpya wa Simba, Ibrahim Ajibu na Francis Kahata wamekiona cha moto ni baada ya Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems kutumia saa mbili sawa na dakika 120 kuwakimbiza nyota hao. Hiyo, ikiwa ni saa chache tangu timu hiyo itue Sauzi na kuweka kambi kwenye moja ya hoteli nyota tano ya Royal Marang Hotel ya nchini huko ikijiwinda na Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Bara. Ajibu alijiunga na Simba hivi karibuni akitokea Simba mara baada ya mkataba wake kumalizika wa kuichezea timu hiyo huku Kahata yeye amejiunga na timu hiyo baada ya mkataba kumalizika Gor Mahia ya nchini Kenya. Ibrahim Ajibu atakaa siku sita tu katika kambi yao ya Afrika Kusini kisha atarejea hapa na kujiunga na Taifa Stars. Meneja wa timu hiyo Patrick Rweyemamu alisema mara baada ya kutua huko juzi Jumatatu walifanya program moja ya mazoezi ya jioni kwa kutoa uchovu wa safari lakini siku iliyofuata walifanya mara mbili asubuhi na jioni. Rweyemamu alisema, programu waliyoanza...