HUYU NDO KANOUTE
Sadio Kanoute amekuwa ni miongoni mwa wachezaji waliozungumzwa sana baada ya mechi ya juzi dabi ya Kariakoo kati ya Simba vs Yanga, swali ni je ataendelea kutoa kile alichokitoa juzi katika mechi zijazo za Simba?. Iko hivi, uhalisia uliopo watu wengi hawamtazami Kanoute kama mchezaji mzuri anaeweza kuifanya Simba kuwa imara katika eneo la kiungo, binafsi naamini ni mchezaji mzuri ambae anahitaji muda ili kuwa bora zaidi. Kama unategemea kuona Kanoute akicheza mpira wa kukufurahisha hatakuwa mchezaji mzuri machoni mwako, yeye anatekeleza majukumu yake kimbinu na ni hapa tu ambapo watu wengi wanampa thamani ndogo kwa sababu hana mambo mengi. Ubora alioonyesha jana unaweza kuwa ni mwanzo wa kumfanya aendelee kuwa imara zaidi, kama mchezaji anaweza kucheza katika presha kubwa kama ya jana na ikapelekea azungumzwe kwa mazuri hiyo inamjenga vizuri kisaikolojia, kila la kheri kwake. #simbasctanzania #NBCPremierLeague #wingi_van_moses_ZONE