PRISON MABINGWA KOMBE LA HISANI YAIPIGA YANGA 3-1
Picha kwa hisani ya BIN ZUBERY
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania, Godfrey Simbeye, akimkabidhi Kombe, Nahodha wa timu ya Tanzania Prisons, Laurian Mpalile, baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Yanga U20 katika mchezo wa Hisani wa fainali wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS, Dk. Leonard Maboko (kulia kwake) ni Katibu wa TFF Mkoa wa Mbeya, (kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS, Elizabeth Kaganda.
Kiungo wa Yanga B, Said Mussa (kushoto) akiudhibiti mpira mbele ya mchezaji wa Tanzania Prisons, Mohamed Rashid kwenye mchezo huo
Beki wa Tanzania Prisons, James Mwasote akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga B, Samuel Greyson
Mshambuliaji wa Yanga B, Festo Geryson (kushoto) akiwania mpira wa juu na beki wa Tanzania Prisons, James Mwasote
Wachezaji wa Prisons katika picha ya pamoja na Medali zao jana Uwanja wa Sokoine
Maoni
Chapisha Maoni