SIMBA KUTESTI MITAMBO SIKU YA LEO



Johannesburg,Afrika Kusini.

MABINGWA wa kombe la FC,Simba SC leo Jumanne wanatarajiwa kucheza mechi yao ya kwanza ya maandalizi ya msimu mpya kwa kuvaana na mabingwa wa zamani wa Afrika,Orlando Pirates ya Afrika kusini. 

Orlando Pirates ambayo ndio klabu maarufu zaidi nchini humo,imeahidi kushusha silaha zake zote muhimu ili kuwapa maandalizi ya kutosha Simba SC.Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye dimba la Orlando liliopo jijini Johannesburg. 

Mechi nyingine ya mwisho itakayochezwa na Simba SC nchini humo itapigwa siku ya Alhamisi ya wiki hii dhidi ya mabingwa wa soka nchini humo kwa sasa Bidvest Wits wanaochezewa na kiungo wa zamani wa Everton na Sunderland, Steven Piennar.

Wakati huohuo Simba SC wamethibitisha kumsajili mlinda mlango Aishi Manula kutoka Azam FC kwa mkataba wa miaka miwili.

Mlinda mlango huyo anayeichezea pia timu ya taifa ya Tanzania,kesho Jumanne ataungana na wachezaji wenzake walioweka kambi huko Eden Vale Johannesburg, nchini Afrika kusini. 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MBARAKA YUSUPH BADO HALI TETE

NIYONZIMA AAHIDI ZAWADI KWA KAZIMOTO