TFF KUZIPUNGUZIA MZIGO SIMBA NA YANGA

Dar es Salaam. Kamati ya utendaji ya shirikisho la soka Tanzania (TFF), imezipunguzia mzigo za Ligi Kuu baada ya kuridhia kupunguza ada inayolipwa kwa wachezaji wa kigeni wanaosajiliwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF leo, kila mchezaji wa kigeni anayesajiliwa na klabu inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara sasa atalipiwa ada ya Shilingi milioni mbili tofauti na hapo awali ambapo kanuni ilitaka kila mchezaji wa kigeni alipiwe ada ya Dola 2000 (Sh.4.5 milioni).
Mabadiliko mengine ya kanuni ambayo kamati ya utendaji ya TFF imeyaridhia ni kutotambuliwa kwa mkataba wa mchezaji ambao haujasajiliwa na shirikisho hilo sambamba na wachezaji kukatiwa bima za afya.
Masharti hayo ni kukatiwa Bima ya Matibabu, Kuidhinishwa afya yake ambayo mara baada ya fomu yake kupitishwa na Kamati ya Tiba ya TFF kwa mujibu wa Kanuni ya 18 (1) ya Ligi Kuu na Mkataba wake wa maandishi ‘hardcopy’ kuwasilisha TFF kwa mujibu wa Kanuni ya 69 (8) ya Ligi Kuu.
Kama kuna timu haitakidhi japo sharti moja kati ya hayo, basi mchezaji wake hatapewa leseni ya kucheza kwa msimu husika.
Wakati huohuo kikao hicho cha kamati ya utendaji ya TFF kimetangaza ukumbi ambao mkutano mkuu wa shirikisho hilo utafanyikia Agosti 12 mjini Dodoma ambapo ajenda yake kuu itakuwa ni uchaguzi mkuu wa TFF.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF, mkutano huo utafanyika kwenye Ukumbi wa St. Gasper ambao uko kilometa saba (7) kutoka mjini Dodoma.
Aidha, Kanuni ya 14 imeongezwa kipengele kimoja. Kanuni ya 14 (48) Klabu ina wajibu wa kushirikiana na mdhamini wa matangazo ya televisheni ikiwemo kupata picha za wachezaji na benchi la ufundi kwa ajili ya maandalizi ya mechi zao.
Na Kanuni 14 (49), inasema: TFF/TPLB itachukua hatua kwa ukiukwaji wo wote wa taratibu za mchezo kama zilivyoanishwa kwenye Kanuni ya 14 kwa kutoa onyo kali au karipio au kutoza faini kuanzia Sh. 200,000 mpaka Sh. 300,000, na/au kufungia mchezo isiyozidi mitatu (3) au kipindi kisichozidi miezi mitatu (3) kwa mchezaji, kiongozi au timu

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MBARAKA YUSUPH BADO HALI TETE

NIYONZIMA AAHIDI ZAWADI KWA KAZIMOTO