"SIMBA WEEK" KUTINGA TAASISI YA MOYO YA JK
Maadhimisho ya siku maalum ya klabu ya Simba maarufu kama ‘Simba Day’ yanaanza siku ay Jumanne Agosti 01, 2017 na yatakwenda wiki nzima hadi Agosti 8 ambaye ndiyo siku ya kilele.
Katika wiki hiyo itakayofahamika kama ‘Simba Week’, uongozi wa klabu hiyo kwa kushirikiana na mashabiki pamoja na wachezaji wanatarajiwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii, ambapo kwa mwaka huu, moja ya shughuli zitakazofanyika ni kuchangia matibabu ya upasuaji wa kwa watoto wenye matatizo ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Muhimbili Jijini dar es Salaam.
Mratibu wa shughuli hiyo Imani Kajula amesema mbali na kuchangia upasuaji huo, pia viongozi na wachezaji watatembelea taasisi hiyo kubwa ya moyo barani Afrika ndani ya ‘Simba Week’
Pia amesema miongoni mwa shughuli nyingine za kijamii itakuwa ni kutoa misaada malimbali kwa watoto yatima katika vituo vitakavyobainishwa hapo baadaye.
Kauli mbiu ya Simba Day mwaka huu ‘Ki-Simba zaidi’, ambapo Kajula amesema sababu ya kaulimbiu hiyo ni kutokana na Simba kujiongeza katika mambo mengi mwaka huu yanayohusu uendeshaji wake.
“Ki-Simba zaidi ni kaulimbiu inayolenga ongezeko la mambo kadha wa kadha ndani ya Simba” Amesema Kajula
Amesema kauli mbiu hiyo inawahusu pia mashabiki wa Simba ambao wanatakiwa kujiongeza zaidi kwa kuongeza mapenzi na klabu yao ikiwemo kuchangia kwa njia mbalimbali kama vile kununua jezi na kwenda uwanjani huku wakitambua kuwa wao ni Simba.
Katika hatua nyingine, Kajula amesema mwaka huu Simba Day itakuwa na mambo mengi zaidi na kwa mara ya kwanza itasherehekewa nchi nzima, ambapo viongozi wa matawi katika mikoa yote nchini wametakiwa kuandaa sherehe hizo katika mikoa yao.
Maoni
Chapisha Maoni