BOCCO NA OKWI WAMTOA UDENDA MZUNGU WA BIDVEST

Jo'burg, Afrika Kusini. Kocha wa mabingwa wa Ligi Kuu Afrika Kusini, Bidvest Wits FC, Gavin Hunt amesema amevutiwa na viwango vya John Bocco na Emmanuel Okwi ila kinachomtia woga ni dau.
MCL Digital imetinga Bidvest na kujionea mazingira halisi ya klabu hiyo inayomilikiwa na chuo ikizungukwa na viwanja vya soka zaidi ya vitatu kila kimoja kwa ubora wake.
Kocha Hunt alisema siku nyingi wanamtaka Bocco, lakini fedha yake kubwa, Azam walitupa dau ambalo tulishindwa kwenda nao sawa, sasa nilipomwona tena na Simba nimeshangaa na yuko katika ubora wa juu zaidi.
"Mchezaji mwingine ni yule namba saba, Okwi ni mzuri hata leo tunatamani kuwa na mchezaji kama yeye," alisema Hunt.
Akikizungumzia kikosi Simba kwa ujumla, Hunt alisema Simba ni timu nzuri na ina wachezaji wazuri na hasa katika safu yao ya ushambuliaji, Okwi na Bocco (kwa kuwataja majina) wana uelewano mazuri kwenye ushambuliaji.
"Kwa sasa wako kwenye maandalizi na mazoezi magumu, miili ikifunguka watakuwa vizuri zaidi."
Katika mchezo huo na Bidvest ilitoa sare ya 1-1 na Simba huku beki Erasto Nyoni akifunga bao ilo pekee.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MBARAKA YUSUPH BADO HALI TETE

NIYONZIMA AAHIDI ZAWADI KWA KAZIMOTO