GWIJI LA SOKA CAMPBELL ATUA JIJINI
Gwiji la soka Sol Campbell atua jijini
05 Aug 2017, 05:38 pm|
Mashabiki wa gwiji la Arsenal, Sol Campbell mapema leo, Jumamosi walionekana katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), tayari kwa kumpokea mchezaji huyo aliyetikisha katika ulimwengu wa soka kwa muda mrefu.
Mashabiki hao walionyesha kuwa na bashasha wakitaka kumuona mchezaji huyo aliyeiwezesha Arsenal kubeba vikombe enzi zake akiwa beki kisiki.
Campbell ambaye ni raia wa Uingereza anawasili nchini huku akitarajiwa kushuhudia mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Arsenal dhidi ya Chelsea.
Campbell ambaye pia amewahi kuichezea Tottenham Hotspur ya England, katika ziara yake nchini ataendesha mafunzo kwa timu ya Magnet katika Uwanja wa Gymkhana na kutembelea timu ya Muungano kwenye Uwanja Karume
“Huyu ni nyota wa pili wa zamani wa soka baada ya Leon Osman wa Everton, tunajua bado watu wanakumbuka ujio wa Everton huu ni muendelezo wa kuleta hamasa ya soka nchini
Maoni
Chapisha Maoni