KAULI YA KWANZA YA NEYMA JR.
Hii leo mshambuliaji mpya wa klabu ya Psg Neymar Dos Santos ametambulishwa rasmi mbele ya waandishi wa habari na huku akipewa jezi namba 10.
Neymar ameongea mengi kuhusu uhamisho wake huu uliovunja rekodi ya dunia “nilihitaji changamoto mpya katika soka na moyo wangu ulikuwa ukiniambia kwamba Psg ni mahala sahihi kwangu”
“Ilikuwa ni muda sahihi kwangu kuondoka Barcelona na kwenda kutafuta changamoto mpya na nimekuja hapa nikiwa tayari na hata kesho naweza kuanza kucheza” alisema Neymar.
“Nina furaha sana kuvaa jezi ya Paris Saint German na kubeba jina la taifa langu pamoja na mimi, niko tayari kucheza popote kocha atakapotaka nicheze mimi nataka kucheza soka tu”
“Paris Saint German ni klabu ambayo inataka kuja kuwa klabu kubwa duniani na mimi nataka kuwa sehemu ya watu ambao wataandika historia na klabu hii, sikuvutiwa na pesa kuja hapa bali mipango ya klabu hii”
Kuhusu Javier Pastore aliyekubali kumpa jezi namba 10, Neymar alisema “Pastore namshukuru sana kwa kunipa namba hii, naheshimu sana upendo wake kwangu”
Wakati Neymar akisema hayo, mmiliki wa klabu hiyo Nasser Al Khelaifi amesema kwa sasa wanataka kushinda Champions League na sasa wanaenda kupambana kikweli kweli kuhakikisha Psg inabeba kombe hilo.
Nasser pia amesisitiza kwamba PSG haikukiuka sheria za Financial Fair Play za FIFA na kusisitiza kwamba UEFA inajua kila kitu kuhusu usajili wa Neymar na hakuna kitu kilichofichwa
Maoni
Chapisha Maoni