MZUNGU WA ORLAND PIRATES AMPIGIA SARUTI OKWI
JOHANNESBURG. Nani anayesema straika wa Simba, Emmanuel Okwi amekwisha, usirudie tena, kwani kocha mkuu wa Orlando Pirates, Kell Jonevret amesema, hajaona kama yeye na akawasifu Wekundu hao wa Msimbazi kwamba watasumbua sana kwenye Ligi ya Tanzania kutokana na maandalizi yao.
Kocha huyo ambaye alicheza na Simba na kutumia wachezaji tofauti wa kikosi cha kwanza na cha pili.
Alifanya mahojiano na Mwanaspoti ndani ya Uwanja wa Orlando Pirates baada ya mchezo huo kumalizika alisema, “Tumepata majaribio mazuri Simba ni timu nzuri kwani imetupa changamoto kubwa. Hata sisi ndiyo tumeanza maandalizi yetu.”
“Tumewafunga bao moja ambalo halikuwa rahisi wametusumbua, walikuwa wazuri na nafikiri tumeweza kuwafunga kwa sababu inaonekana wamefanya mazoezi magumu, wana uchovu, miili imekaza, maumivu madogomadogo na mambo meengine.”
“Na huu ndiyo mchezo wao wa kwanza hivyo kitaalamu mazoezi ya pre-season lazima iwe hivyo, kwenye mechi ya pili kutakuwa na mabadiliko ninachoamini watacheza vizuri kwa sababu ile hali itakuwa inaondoka.”
Maoni
Chapisha Maoni