SIMBA YATEUA MRITHI WA MGOSI

Simba yateua mrithi wa Mgosi

02 Aug 2017, 07:10 pm| By Ally TegoSOKA TANZANIA

Klabu ya Simba imemteua Dkt. Cosmas Kapinga kuwa meneja mpya wa timu hiyo akichukua nafasi ya Mussa Hassan ‘Mgosi’ ambaye amepangiwa majukumu mengine ndani ya klabu.

Taarifa iliyotolewa na mkuu wa habari na mawasiliano wa Simba, Haji Manara, imeeleza kuwa Kapinga ataanza kazi yake mpya mara baada ya kikosi cha Simba kurejea nchini kutoka Afrika Kusini.

Manara amesema kuwa Mgosi atakuwa kocha msaidizi na meneja wa timu ya vijana akiwa na Nico Nyagawa ambaye naye atakuwa kocha msaidizi wa kikosi hicho.

Amesema kikosi hicho cha vijana kitaendelea kuwa chini ya kocha mkuu Nico kiondo.

Mgosi anatarajia kufanya mafunzo ya ukocha leseni C, ambayo yatampa fursa ya kuongeza ujuzi kwenye majukumu mapya ya ualimu ndani ya timu yetu.

Wakati huo huo, benchi la ufundi la timu hiyo limeridhishwa na maandalizi yao nchini Afrika Kusini, ikiwa ni pamoja na jinsi kikosi kilivyocheza jana licha ya kufungwa bao 1-0 na Orlando Pirates.

“Ingawa tumepoteza mchezo wetu wa jana,lakini tumeshaanza kupata mwelekeo wa kikosi, na katika siku chache zijazo, tayari tutakuwa tumeshapata kikosi cha kwanza" amesema Mwalimu Omog.

Hapo kesho timu hiyo itashuka kwenye dimba la Sturrock Park liliopo ndani ya Chuo Kikuu cha Wits kilichopo Braamfontein jijini Johannesburg kucheza mechi ya mwisho ya maandalizi nchini humo dhidi ya Bidvest.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MBARAKA YUSUPH BADO HALI TETE

NIYONZIMA AAHIDI ZAWADI KWA KAZIMOTO