PSG KUHOJIWA NA FIFA JUU YA FEDHA ZA KUMNUNUA NEYMA JR.

Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) limepanga kuihoji klabu ya PSG ilikozitoa fedha ambazo zitatumika kumsajili nyota wa Barcelona, Neymar Jr. Kiwango hicho cha fedha kimelishtua shirikisho hilo ikiwa ni fedha ya usajili ambayo inatarajiwa kuvunja rekodi ya dunia kwa kumsajiri mchezaji mmoja. Shirikisho hilo limesema kwamba halitasita kuiadhibu klabu hiyo ya Ligue 1 iwapo litabaini kukiuka kanuni za usajili kwa wachezaji.