Machapisho

KAULI YA NIYONZIMA LEO HII MAZOEZINI

Picha
“Najua kuna chuki na maneno ya kejeli yameanza kusemwa juu yangu lakini mimi sijali, ninachowaza ni namna gani naweza kuipa timu yangu mafanikio kwa sababu ndiyo inayoniweka hapa Tanzania na nitajibu maneno yao kwa kutumia miguu yangu na siyo mdomo,”- Haruna Niyonzima Toa maoni yako

SIMON MSUVA KUTUA HISPANIA KWA SIKU SABA

Picha
Dar es Salaam. Winga wa Mtanzania, Simon Msuva amesafiri na kikosi cha timu yake ya Difaâ Hassani El Jadidi kwenda nchini Hispania kuweka kambi ya siku saba. Katika kambi hiyo watakuwa na michezo kadhaa ya kujima ubavu kabla ya kurejea Morocco kwa ajili ya kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu nchini humo 'Batola Pro'. Msuva amesajili na klabu hiyo ya Morocco akitokea Yanga ambayo aliitumikia msimu uliopita.

NIYONZIMA AAHIDI ZAWADI KWA KAZIMOTO

Picha
Niyonzima aahidi zawadi kwa Kazimoto Nyota mpya wa Simba aliyesajiliwa hivi karibuni baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga, Haruna Niyonzima ameahidi kumtafutia zawadi kiungo mkongwe wa klabu hiyo, Mwinyi Kazimoto kutokana na hatua yake ya ‘kumvulia jezi. Kazimoto aliyekuwa akivaa jezi namba 8, ameamua kumuachia kiungo huyo raia wa Rwanda baada ya kuombwa kufanya hivyo kama ishara ya heshima kwake. “Namshukuru sana Mwinyi kwa heshima aliyonipa, na mimi namuahidi kumtafutia zawadi, ni lazima nimzawadie kwa hili alilonifanyia” amesema Haruna Akizungumzia sababu za kuiomba jezi hiyo, Haruna ambaye mara nyingi hucheza kama kiungo namba 8, amesema jezi hiyo ina kumbukumbu kubwa katika maisha yake ya soka, na ndiyo aliyokuwa akiivaa wakati akiwa Yanga Niyonzima ambaye ameanza kuonyesha cheche katika klabu ya Simba kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Rayon Sports iliyopigwa jana kuadhimisha Simba Day, ameahidi kuitumikia Simba kwa nguvu zote katika mechi zote na amesema ataanza na m...

LWANDAMINA AJIPIGA KIFUA JUU YA KIKOSI CHAKE

Picha
Kocha mkuu wa Yanga, Mzambia George Lwandamina ameanza kulidhishwa na maandalizi ya timu yake kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Kikosi hicho cha Lwandamina kitakuwa na kibarua kizito cha kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Bara kuanzia Agosti 27 itakapocheza dhidi ya Lipuli kwenye Uwanja wa Taifa. Yanga ilianza maandalizi ya msimu mpya kwa kufanya mazoezi ya Gym jijini hapa kabla ya kwenda mkoani Morogoro ambapo waliendelea na mazoezi ya kujenga utimamu wa mwili kwa kukimbia na mapalashuti. "Tumejiandaa na tunaweza kuanza ligi, ni wazi kuwa msimu huu utakuwa na ushindani mkubwa kwa sababu timu nyingi zimejiandaa na hata kusajili vizuri," alisema Lwandamina. Katika mazoezi ya leo asubuhi kwenye Uwanja wa Polisi Kurasini, kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa alikuwa akitilia mkazo namna ya ukabaji. Yanga inajiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba utakaofanyika Agosti 23, jambo lililomfanya Nsajingwa kuwa mkali kwa makosa ya kizembe yaliyokuwa yaki...

PSG WAMNYAPIA ALEXIS SANCHEZ

Picha
Arsene Wenger ameelezea mstari ambao Alexis Sanchez hauzi kuuzwa wakati wa majira ya joto, lakini Ripoti ya Independent ya kwamba Paris Saint-Germain itafanya hoja kubwa zaidi ya £ 80 milioni, wiki tu baada ya kupiga rekodi ya dunia kwa £ 200,000 Senda kwa Neymar. Vigogo vya Ligue 1 vinabaki kwenye soko kwa mshambuliaji na wanaendelea kufuatilia Kylian Mbappe, lakini Sanchez bado ni lengo la juu. Chile inaaminika kuwa tayari kukaa baada ya uamuzi wa Gunners kumsimamia, licha ya mwaka mmoja tu iliyobaki kwenye mpango wake. Baada ya kugonga tena mpango mpya wa thamani ya £ 250,000 kwa wiki ili kupanua kukaa kwake kwa Emirates, PSG itatoa £ 400,000 kwa wiki kwa jitihada za kumshawishi Sanchez kuwachagua juu ya Manchester City. Lakini tamaa ya Sanchez ya kufanya kazi na Pep Guardiola ni kwamba mji huo unaaminika kuwa unaweza kukubaliana na masharti ya mkataba mpya wa mkataba wa Gunners.

OBREY CHIRWA AMESHAIVA KIBONGO

Picha
Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa ameanza kuiva bana katika uzungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Chirwa anaweza kufanya mawasiliano na wachezaji wenzake kwa Kiswahili japo anaongea kama mtu mwenye kigugumizi katika utamkaji wa maneno lakini anaonekana kuanza kukifahamu vizuri. Kuna muda staa huyo wa Yanga huwa anachanganya maneno pale anaposhindwa kutumia neno fasaha la Kiswahili. Mzambia huyo amedai kuwa karibu na wachezaji wenzake, kumemfanya kukifahamu Kiswahili kwa haraka. "Muda mwingi huwa nasikia Kiswahili kikizungumuzwa na wachezaji wenzangu huwa najifunza, sio kwamba hii ni lugha ni ngumu hapana,"alisema Chirwa.

BALOTELLI APATA MSALA MWENGINE

Picha
Unaweza ukasema, yaleyake. Mario Balotelli hakui maana kila siku, vituko tu. Safari ameng’ang’aniwa na Polisi baada ya kuendesha gari lake mwendo kasi kupitiliza hadi kufikia mail 125 kwa saa. Balotelli alikuwa akiendesha gari aina ya  Ferrari, amekamatw ana Polisi nchini Italia. Mshambuliaji huyo wa Nice ya Ufaransa, alikuwa akikimbia kwa kasi hiyo huku akijua hairuhusiwi kufanya hivyo. Polisi hao waliokuwa katika eneo la Vicenza walifanikiwa kumkimbiza na kumsimamisha kabla ya baadaye kumkamata. Moja ya faini aliyopigwa ni kwa kuwa gari lake limesajiliwa mwendo mkubwa kuwa ni maili 105 kwa saa na si zaidi.