TUNALIAMSHA DUDE TAIFA

Ile siku iliyokua ikingojewa na wapenzi wengi wa soka la bongo hasa mashabiki wa timu kubwa mbili za hapa nchini,yaani hapa namaanisha ile Derby ya Kariakoo hatimae imewadia. Leo ni leo katika Uwanga wa taifa ambapo tutashudia vidume na vigogo wa soka nchini wakishuka dimbani kumenyana katika mchezo wa Ngao ya Hisani ikiwa ni ishara ya kufunguliwa kwa pazia la ligi kuu Vodacom Tanzania ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vimba Jumamosi hii katika viwanja mbalimbali hapa nchini. Miamba hao wa soka nchini (Simbana Yanga) wanatarajiwa kushuku dimbani mida ya Saa 11:00 jioni ya leo kucheza mchezo huo huku presha ikizidi kuongezeka kila wakati. Wakuu wa vitengo vya habari wa timu zote wamethibitisha vikosi vyao kua imara na kua tayari kwa mtanange huo licha ya mapungufu walio nayo. Mpendwa msomaji wa vyankende.com ikumbukwe kua baadhi ya wachezaji wa Yanga hawatacheza mchezo huo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na majeruhi na yule aliekutana na rungu la TFF.Na kwa upande wa Simba mpa...