TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 01.08.2017 Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28, hatojiunga na kikosi cha kwanza kwa ajili ya kuanza mazoezi siku ya Jumanne huku akiendelea kufuatilia uhamisho wake kuondoka Stamford Bridge. (Marca) Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri ameiambia Chelsea kuwa hawatomuuza beki wa kushoto Alex Sandro, 26. (Sport Mediaset) Meneja wa Chelsea Antonio Conte anataka kumsajili kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater, 27, baada ya Nemanja Matic kwenda Man Utd. (Mail) Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp huenda akaamua kumfuatilia kiungo wa Bayern Munich Renato Sanches, 19, iwapo Philippe Coutinho, 25, ataondoka kwenda Barcelona. (Bild) Bayern Munich wamekataa dau la pauni milioni 10 kutoka kwa AC Milan wanaomtaka Renato Sanches, 19, kwa mkopo. (Le10Sport) Beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26, atakuwa na mazungumzo na meneja wake mpya Mauricio Pellegrino, wiki hii, huku Liverpool wakijiandaa kuvunja rekodi yao ya usajili kumchukua beki huyo wa kimataifa ...