Kampala, Uganda. Orlando Pirates ipo tayari kumnunua beki wa Uganda, Simba SC, Murushid Juuko kwa mujibu wa KickOff.com. Beki huyo wa Uganda, Juuko ameripotiwa kuwa yuko njiani kujiuanga na miamba hiyo ya Soweto, Orlando Pirates. Beki huyo mwenye miaka 23, kwa sasa yupo na kikosi cha Simba kinachojiandaa Afrika Kusini alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Uganda Cranes walioshiriki katika Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 nchini Gabon. Kwa mujibu wa vyanzo vya kuhaminika kutoka Uganda, Juuko alisema amekuwa akifuatiliwa na Buccaneers, ambaye wanatakiwa kununua mkataba wake wa miezi minne uliobaki na Simba. "Murushid Juuko amehusishwa na kutakiwa na Orlando Pirates,” chanzo hicho kimeimbia KickOff.com. “Ni beki mzuri anayecheza katika klabu ya Simba SC." Aliendelea kuwa: "Juuko amebakiza miezi minne katika mkataba wake wa sasa. Hivyo ni bora Simba wakakubali kuuza sasa au la kumwacha ondoke bure.”